32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

BYAKANWA AWAWAKIA WANAOWAPA WANAFUNZI KINGA ZA UJAUZITO

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gellasius Byakanwa ameshangazwa na tabia ya wanafunzi wa kike mkoani humo kutumia kinga kuzuia ujauzito.

Kutokana na hali hiyo, amezitaka mamlaka husika kuzichukulia hatua maduka na zahanati zinazohusika kutoa huduma hiyo kwa watoto wenye umri chini ya miaka 14.

Akizungumza katika kikao cha wadau wa elimu mkoani hapa Byakanwa amesema kitendo cha watoto wa kike kutumia kinga hizo kinaonyesha wazi kuwa wazazi wameacha jukumu la kusimamia watoto.

Amesema kitendo hicho ni matokeo ya watoto kujilea wenyewe kutokana na mihangaiko ya maisha wazazi wanakosa muda hali ambayo inachangia wingi wa mimba kwa watoto wenye umri wa miaka 14 hivyo kuhatarisha maisha ya watoto hao.

“Mfano unaenda Wilaya ya Nanyumbu unakuta watoto wa kike wanatumia kinga ya kuzuia mimba hii ni laana siyo kwao tu hata kwa hao wanaohusika kutoa hizo kinga nazitaka mamlaka husika kufuatilia hayo maduka yanayouza hizo kinga kwa mtoto wa kike tena wanafunzi, chukueni hatua….

“Hatuwezi kuufumbia macho ulegevu wa wazazi kushindwa kusimamia watoto wao unakuta mtoto wa kike hapati siku zake mzazi hahoji wala hafuatilii wakati yeye ndiyo mwenye jukumu la kumnunulia mtoto huyo vitambaa vya kujikinga kwanini hahoji hilo,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Byakanwa ameagiza watoto wa kike wa shule za msingi na sekondari kupimwa ujauzito kila wanapoanza shule ili kujua takwimu halisi na wanaokutwa na mimba wakae pembeni kama Rais John Magufuli alivyoagiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles