33.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

CCM YAFUTA MCHAKATO KURA ZA MAONI KWA NYALANDU

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimefuta mchakato wa kura ya maoni uliofanyika katika Jimbo la Singida Kaskazini, kutokana na baadhi ya wagombea kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya mfanyabiashara Haider Gulamali, kuibuka mshindi kwenye kura hizo, kugombea nafasi ya kuiwakilisha chama hicho katika kuwania jimbo hilo lililoachwa wazi na Lazaro Nyalandu tangu Oktoba mwaka huu baada ya kujivua uanachama wa CCM na kujiunga na Chadema.

Gulamali alipata asilimia 60 ya kura na kuwabwaga wagombea wengine 21 katika kinyang’anyiro hicho, huku Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Elia Digha aliyedaiwa kuwa tishio, akishindwa kurejesha fomu yake kwa muda uliopangwa, hivyo kujiondoa mwenyewe.

 

MCHAKATO WAFUTWA

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, mchakato mpya wa kura hizo za maoni utaanza tena leo kwa kuchukua na kurudisha fomu za maombi ya kushiriki kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 12 jioni.

“Wanachama wa CCM wanaotaka kugombea Singida Kaskazini wachukue fomu na kurejesha. Siku ya Alhamisi Desemba 14 mwaka huu, itapigwa kura ya maoni na Halmashauri Kuu ya Jimbo badala ya Mkutano Mkuu wa Jimbo ili kuwahi mchakato.

“Wanachama wa CCM wanajulishwa kuwa Haider Gulamali na Elia Mlangi hawaruhusiwi kugombea nafasi ya ubunge wa Singida Kaskazini kupitia CCM kutokana na tuhuma nzito za kujihusisha na vitendo cha rushwa,” ilisema taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles