25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

DK. NDUNGULILE ‘ANUSA JIPU’ MSD

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile amewapa siku mbili Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Dk. Said Mawji na Meneja wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Herman Mng’ong’o kujieleza kwanini fedha nyingi za dawa zinatumika kununua dawa nje badala ya MSD kama serikali ilivyoelekeza.

Amesema taarifa aliyopatiwa inaonesha dawa nyingi wanazotumia hospitalini hapo hazitoki MSD, zinanunuliwa nje kati ya milioni 57 ambazo zimeripoti Sh 78,000 tu ndizo zimekwenda MSD milioni 50 zimekwenda nje.

“Kwa maelezo yote tuliyopewa hapa kwa mujibu wa Meneja wa MSD dawa nne tu ambazo hazipo kwenye bohari yao mwezi Oktoba, mwaka huu.

“Maana yake dawa nyingine zote mlizonunua hapa zilipaswa kuwa MSD nataka maelezo ya kina kwa nini mlinunua dawa nje ya mfumo wa MSD wakati zilikuwepo,” amesema.

Dk. Ndungulile amesema wanatarajia dawa zote muhimu zaidi ya 135 zipo katika bohari za dawa lakini kama wanaenda tofauti na hapo maana yake kuna tatizo na ambalo MSD wanashiriki.

“Katika hili leteni taarifa, naomba msinidanganye maana na mimi nitatafuta ripoti yangu, haiwezekani zaidi ya asilimia 80 ya fedha zinatumika nje wakati MSD dawa zipo,” amesema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles