26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kina Mramba kuhukumiwa Juni 30

mafisadiNa Kulwa Mzee, Dar es Salaam

HUKUMU ya kesi inayowakabili aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona na wenzao inatarajiwa kusomwa Juni 30, mwaka huu, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Uamuzi huo ulifikiwa jana, mbele ya jopo la mahakimu watatu, likiongozwa na Jaji John Utamwa, baada ya kupangwa kwa tarehe za majumuisho ya mwisho wa kesi hiyo. Mahakimu wengine katika kesi hiyo ni Sam Rumanyika na Saul Kinemela.

Mbali na Mramba na Yona, mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo iliyochukua takriban miaka saba ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.7 kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni iliyopata zabuni ya ukaguzi wa madini ya dhahabu nchini ya M/S Alex Stewart.

Upande wa utetezi na ule wa Jamhuri umepangiwa tarehe za kuwasilisha majumuisho yao ya mwisho iwapo wanaona washitakiwa wana hatia au la, baada ya kukabidhiwa mwenendo wa kesi hiyo Jumatatu, wiki ijayo ambapo utakuwa umeshakamilika kuchapwa.

Mahakama hiyo iliuamuru upande wa utetezi kuwasilisha hoja zao Juni 9, mwaka huu na upande wa Jamhuri kuwasilisha majibu ya hoja za utetezi Juni 17, mwaka huu, huku upande wa utetezi iwapo utakuwa na majibu ya nyongeza kuwasilisha kabla ya Juni 25, mwaka huu na hukumu itatolewa Juni 30, mwaka huu.
Wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo, upande wa Jamhuri uliita mahakamani hapo mashahidi saba na baada ya kufunga ushahidi wao, washitakiwa walionekana wana kesi ya kujibu, hivyo kutakiwa kutoa utetezi wao.

Kwa upande wa utetezi, walitoa ushahidi wao wenyewe wakiwa na mashahidi wao wawili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles