25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Sugu ataka jimbo lake lisigawanywe

Joseph-Mbilinyi-SuguNa Debora Sanja, Dodoma

MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), ameitaka Serikali kumhakikishia kwamba hawataligawa jimbo lake kwa kuwa kufanya hivyo ni sawa na kugawa moyo wake.
Akiuliza swali la nyongeza bungeni jana, Mbilinyi maarufu kama Sugu
alisema haoni sababu ya kugawa jimbo lake kwa kuwa hata wakati
anagombea alijua kwamba jimbo hilo ni kubwa.
Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Uratibu na Bunge, Jenister Mhagama alisema matakwa ya kuligawa jimbo hayazingatii maslahi ya mbunge wa jimbo husika.
“Ili kuligawa jimbo vipo vigezo vya utawala vinavyoangaliwa, kama
jimbo la Mbeya litakuwa limekidhi vigezo hakuna jinsi litagawanya kwa
mahitaji ya utawala bora,” alisema.
Alisema kama wapo wabunge hawataki majimbo yao yagawanye pamoja na kwamba yamekidhi vigezo hawawatendei haki wananchi wao kwa misingi ya utawala bora.
Kwa upande wake Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keisy Mohamed (CCM),alilalamikia ugawanyaji wa majimbo kwa upande vwa Zanzibar kwamba hautendi haki kwa kuwa majimbo yake ni madogo na watu wake ni wachache.
Mhagama alisema mfumo wa kugawa majimbo Zanzibar unazingatia taratibu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
“Lakini hata hivyo kama Mheshimiwa Keisy anaona jimbo lake ni kubwa namshauri aende akagombee Zanzibar,” alisema.
Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Njombe Kaskazini, Deo Sanga (CCM), Mhagama alisema kwa kuwa Mkoa wa Njombe umependekeza kuligawa Jimbo la Njombe Kaskazini, NEC inaweza kuligawa jimbo hilo endapo litakidhi vigezo.
Katika swali lake, Sanga alitaka kujua kama jimbo lake litagawanywa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles