25.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

WAKULIMA WA KOROSHO WAZIDI KUKUMBUSHWA

Na HADIJA OMARY-LINDI


WAKULIMA wa korosho mkoani Lindi, wametakiwa kuongeza umakini katika uchambuaji na uwekaji wa madaraja korosho zao ili kuendelea kupata bei nzuri.

Ushauri huo umetolewa jana na Katibu Tawala Msaidizi, Uchumi na Uzalishaji, Mkoa wa Lindi, Majid Myao, alipokuwa akizungumza kwenye mnada wa korosho uliofanyika katika Kijiji cha Mvuleni katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini, Mkoa wa Lindi.

“Siri kubwa ya wakulima kuendelea kupata bei nzuri katika zao hilo ni kuziweka korosho zao katika madaraja yatakayozifanya ziendelee kuwa katika hali nzuri.

“Kama hilo halitazingatiwa, kuna uwezekano bei ya korosho ikashuka kwa kuwa bei inakuwa kubwa kwa sababu ya ubora wa korosho,” alisema.

“Nina furaha kuona bado bei ya korosho iko juu kwani mpaka sasa huu ni mnada wa nne, ambapo bei ya juu ni shilingi 4,800 kwa kilo na bei ya chini ni shilingi 3,980 kwa kilo.

“Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani korosho zetu zimekuwa na ubora wa kutosha tofauti na miaka iliyopita,” alisema Myao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Lindi Mwambao kinachounganisha Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Lindi Vijijini na Wilaya ya Kilwa, Abdallah Mtajenga, aliwataka wakulima wa zao hilo kuendelea kutunza mikorosho yao pamoja na kupanda miche mipya ili waweze kupata mafanikio zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles