27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

JUBILEE WASISITIZA UCHAGUZI, NASA HAKUNA UCHAGUZI

NAIROBI, KENYA


CHAMA cha Jubilee kimeimarisha kampeni yake ya kuomba kura na kutoa wito kwa wananchi wa Kenya kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 26.

Wakati Jibulee kikitoa wito huo, NASA kwa upande wake kinaendelea na kampeni ya kuwahamasisha wananchi kutoshiriki kwenye uchaguzi huo iliyopewa jina la ‘hakuna uchaguzi.’

Wakati mnyukano huo wa kisiasa ukiendelea baina vyama hivyo, tayari shehena ya kwanza ya karatasi za kupiga kura kwa ajili ya kaunti 10 ziliwasili mjini hapa kutokea Dubai juzi Jumamosi.

Vifaa kwa ajili ya kaunti 22 vinatarajia kuwasili leo asubuhi na shehena ya mwisho kwa ajili ya kaunti 15 itawasili kesho.

Rais Uhuru Kenyatta, juzi alifanya mikutano yake ya kampeni huko Kitengela katika Kaunti ya Kajiado na mkutano wake wa awali huko Olkurto katika kaunti ya Narok ukifutwa kutokana na mvua na hali mbaya ya hewa.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, akiwa ameongozana na vinara wenzake, juzi alihudhuria mazishi huko Bondo na mgombea urais wa Thirdway Alliance Ekuru Aukot akiwa Kaunti ya Nakuru.

Kenyatta alisema uchaguzi utaendelea kama ulivyopangwa.

“Iwapo Odinga aliyeenda mahakamani na kufanikiwa maombi yake ya kurudiwa uchaguzi hatashiriki, tutasikitika, lakini lazima tuendelee na uchaguzi huu. Hatuwezi kuwaweka wakenya njia panda kiasi hiki,” alisema Rais Kenyetta akiwa Kajiado.

Kinara mwenza wa Nasa na kiongozi wa Chama cha Amani National Congress (ANC), Musalia Mudavadi alikuwa Lugari, aliituhumu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuishinikiza Nasa ishiriki uchaguzi huo.

Alisema IEBC na Jubilee zote lazima zifahamu msimamo wa upinzani wa kutaka mageuzi kabla ya chaguzi hauhusiani na watu binafsi ndani ya Nasa.

Timu ya Nasa jana ilikuwa Kaunti ya Trans Nzoia na leo itakuwa Kaunti ya Kisii.

Rais Kenyatta na Naibu Rais William Ruto walishiriki ibada ya kuliombea taifa kwenye Uwanja wa Afraha mjini Nakuru jana na leo wataendesha kampeni mjini Nairobi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles