30.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

UMEME KICHOCHEO KWA UCHUMI – TANESCO

NA OSCAR ASSENGA – TANGA

NISHATI ya umeme imeelezwa kuwa ni kiungo muhimu katika kuchochea uwekezaji wa viwanda nchini na utasaidia kuinua kwa kasi uchumi wa Watanzania.

Hayo yalielezwa na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Dk. Tito Mwinuka, juzi katika Baraza Kuu la 47 la wafanyakazi wa shirika hilo  mjini hapa, ambapo alisema kwa kutambua umuhimu huo wanatahakikisha  malengo ya uchumi wa viwanda yanatimia.

Alisema watahakikisha umeme wa uhakika unapatikana katika maeneo mbalimbali nchini bila vikwazo vya namna yoyote ili azma hiyo iweze kutimia kwa vitendo na hivyo kuchochea kasi ya uchumi.

“Kama mnavyojua Serikali ya Awamu ya Tano imeazimia kukuza uchumi wa viwanda, hivyo nishati ya umeme ni kiungo muhimu katika kuchochea uwekezaji wa viwanda ambao utasaidia harakati za maendeleo,” alisema.

“Hivyo napenda kuihakikishia Serikali kwamba tunatambua wajibu tulionao katika kutimiza malengo hayo kwa kuongeza uwajibikaji na ufanisi

kazini ambao ndio utakuwa dira ya kufikia mafanikio,” alisema.

Kaimu Mkurugenzi huyo alisema tangu  kuanzishwa kwake, baraza hilo limekuwa ni sehemu muhimu kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali kwa masilahi ya wafanyakazi ambao wamewaamini kuwawakilisha.

“Baraza hili limesaidia shirika kujua changamoto na kero zinazowakabili mahali pa kazi na kwa pamoja ufumbuzi wake na changamoto hizo zimepatiwa ufumbuzi kwa faida ya wafanyakazi na shirika kwa ujumla,” alisema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles