25.8 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

NEYMAR AITAKA BARCELONA KUFUNGIWA UEFA

PARIS, UFARANSA


MSHAMBULIAJI wa klabu ya PSG, Neymar do Santos, amekiomba Chama cha Soka barani Ulaya (UEFA) kuifungia klabu yake ya zamani ya Barcelona katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na kushindwa kumlipa bonasi yake ya pauni milioni 23.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Hispania, mchezaji huyo alitakiwa kupewa pauni milioni 23 ambazo ni zaidi ya bilioni 66 za Kitanzania kutokana na uhamisho wake wa pauni milioni 198 uliofanyika wakati wa majira ya joto.

Mwanasheria amemshawishi mchezaji huyo kuchukua hatua kali haraka iwezekanavyo dhidi ya klabu yake hiyo ya zamani kutokana na kushindwa kutekeleza kila kilichopo kwenye mkataba wao.

Hata hivyo, Barcelona wenyewe wamesema kwamba hawawezi kutoa fedha hizo kwa kuwa makubaliano hayo yalifanyika wakati tayari amejiunga na kikosi cha PSG, hivyo makubaliano ya awali yalisema kuwa angeweza kupewa fedha hizo kabla ya uhamisho wake kukamilika.

Hata hivyo UEFA imekataa ombi la mchezaji huyo kuifungia klabu ya Barcelona kutoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mkurugenzi wa klabu ya Barcelona, Raul Sanllehi, ametishia kuondoka Camp Nou kutokana na uongozi kushindwa kumzuia Neymar kuondoka wakati huu wa majira ya joto.

Sanllehi ndiye ambaye alipambana na kuhakikisha mchezaji huyo anajiunga na Barcelona akitokea Santos, hivyo ameweka wazi kuwa miaka 15 aliyofanya kazi ndani ya klabu hiyo inatosha ni bora atafute sehemu nyingine.

Mwaka jana Sanllehi alimzuia Neymar kujiunga na PSG, lakini mwaka huu Barcelona walishindwa kuyafanya yale ambayo kiongozi huyo alitaka wayafanye.

Hata hivyo, Barcelona wamesema kuwa wanataka kumalizana na kiongozi huyo kwa urafiki bila ya mgogoro wowote kutokana na mchango wake wa mafanikio makubwa katika kipindi chake chote.

Neymar ndani ya klabu ya Barcelona alikuwa na mchango mkubwa sana katika mafanikio ya klabu hiyo ndani ya misimu minne aliyokaa.

Uhamisho wake umekuwa wa historia katika ulimwengu wa soka kwa kumfanya awe mchezaji wa kwanza kusajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha duniani cha zaidi ya bilioni 568.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles