29.5 C
Dar es Salaam
Monday, September 30, 2024

Contact us: [email protected]

USHER KUWAFUTA CHOZI LAS VEGAS

LAS VEGAS, MAREKANI


MKALI wa muziki wa R&B nchini Marekani, Usher Raymond, anatarajia kuwafuta machozi mashabiki wa muziki mjini Las Vegas, baada ya mashabiki 59 kupoteza maisha na wengine 500 kujeruhiwa kwenye tamasha la Route 91 Harvest Festival wiki iliyopita.

Msanii huyo ambaye anatamba na wimbo wa ‘Stay’, amedai kuwa hahitaji kulipwa chochote ila lengo lake ni kuhakikisha anawasahaulisha mashabiki tukio hilo kubwa la kushambuliwa kwa risasi.

“Siku zote muziki ni sehemu ya watu ambao wanataka upendo, tukio lililotokea wiki iliyopita limewagusa wengi duniani, lakini tutaendelea kufanya shoo kwa ajili ya mashabiki wetu.

“Natarajia kufanya shoo mjini Las Vegas hivi karibuni kwa ajili ya kuwafuta machozi wale waliopoteza ndugu zao na kuguswa na tukio hilo pamoja na kuwaombea waliopoteza maisha,” alisema Usher.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles