27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

SAA MBILI ZA LEMA, NASSARI, MSIGWA TAKUKURU

Wabunge wa Godbless Lema, Joshua Nassari na Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), wametumia zaidi ya saa mbili katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwasilisha ushahidi wa namna madiwani wao walivyoshawishiwa kwa rushwa na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wabunge hao waliingia katika Ofisi za Takukuru jijini Dar es Salaa, saa 8:39 mchana na kutoka saa 10:10 jioni ambapo walisema wamekutana na Mkurugenzi wa Takukuru ambaye amewaeleza tayari uchunguzi wa suala hilo umeanza.

“Tunashukuru tumemkuta Mkurugenzi Valentino Mlowola na timu yake na wametupa ushirikiano wa kutosha, wameniambia nifungue jalada kesho au siku yoyote nitakayoona inafaa na ili jalada lifunguliwe ni lazima niweke watu nilioshirikiana nao katika uchunguzi wangu, tunategemea rais baada ya kuona haya atachukua hatua kwani wateule wake walimdanganya,” amesema Nassari ambaye pia ni Mbunge wa Arumeru Mashariki.

Kwa upande wa Lema amesema: “Leo tumewasilisha sehemu tu ya ushahidi, ila uchunguzi rasmi umeshaanza mkurugenzi ametuambia tusiwe na wasiwasi ile ni taasisi huru ya serikali inayofanyia kazi hata tetesi ingawa kiilichotokea Arusha kilikuwa kweli.”

Naye Mchungaji Msigwa amesema ameambatana na wabunge wenzake hao kwa sababu kilichotokea mkoani Arusha ndicho kilichotokea Iringa ambapo baadhi ya madiwani alinunuliwa.

“Iringa nako biashara kama hiyo ilihusika na Mkuu wa Wilaya na baadhi ya wawakilishi wa rais, lakini pia vifaa vilivyotumika Arusha vimetoka Marekani sisi vyetu vimetoka Australia tutaleta ushahidi wetu pia,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles