30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

UPASUAJI NYONGA, MAGOTI WAANZA KUFANYIKA NCHINI

Na Mwandishi Wetu -Dar es Salaam

HOSPITALI ya Regency ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Hospitali ya HCG Multi Specialty Ahmedabad ya India imeanza upasuaji wa magoti na nyonga nchini ili kuwasaidia Watanzania wasilazimike kwenda nje ya nchi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Hospitali ya Regency, Dk. Rajni Kanabar, kuanza kwa upasuaji huo ni hatua nzuri itakayosaidia Watanzania wengi waliokuwa wakienda kutibiwa nje kutibiwa nchini.

“Hadi sasa tumeshawafanyia upasuaji wagonjwa wanane ambao wamesharuhusiwa wakiwa hawana shida yoyote ile, haya ni mafanikio makubwa kwa hospitali binafsi kuanza kufanya upasuaji wa aina hii unaohitaji utaalamu wa hali ya juu,” alisema Dk. Kanabar.

Pia alisema upasuaji huo umekuwa ukifanywa kwa ushirikiano baina ya madaktari bingwa, Dk. Deepak Dave na Dk. Yuvraj Lakum, wakisaidiwa na wahudumu wa afya wa Regency.

Dk. Kanabar alisema upasuaji huo hufanywa kwa kutumia teknolojia ya kisasa na ya hali ya juu kiasi kwamba mgonjwa anakaa muda mfupi hospitali na kuruhusiwa kwenda nyumbani tofauti na ilivyokuwa zamani.

“Tunachukua wagonjwa wote kutoka kwenye kampuni zinazotumia bima na watu binafsi na kampuni kubwa na upasuaji kama huu utakuwa unafanywa kila baada ya wiki sita hapa Regency. Hii ni fursa ya kipekee kwa Watanznaia kufanyiwa upasuaji wa aina hii hapa hapa Tanzania badala ya kwenda nje,” alisema.

Alisema uchunguzi wa wagonjwa wenye matatizo ya nyonga na magoti utafanyika kuanzia Oktoba 1-3, mwaka huu na upasuaji utafanywa kwa watakaochaguliwa na kuonekana wanahitaji huduma hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles