29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

HAKUNA MDAU WA MITINDO ANAYEWEZA KUMUONYA SANCHI?

KUNA binti anaitwa Jane Rimoy a.k.a Sanchi. Ni maarufu sana katika mitandao ya kijamii. Ni binti mwenye shepu ya kibantu, sura ya kike na vituko vya mwendawazimu.

Kuna kipindi binti huyu aliwahi kusema kwa mwanaume anayetaka kumuoa awe tayari kutoa kiasi cha shilingi milioni 30 kama mahari. Alivyohojiwa kama yuko ‘serious’. Alisema yuko ‘serious’. Watu wakatazamana kwa mshangao.

Watu wakimwangalia binti wa kuolewa hata kwa elf 25 achana na  hiyo milini 30 anayoiota hivi binti mwenye kuweka picha za utupu mtandaoni, binti mwenye kuropoka lolote linalokuja katika kinywa chake, anaolewaje na mtu makini mwenye kujielewa?

Achana na hizo. Tatizo linakuja binti huyu pale anapojitambulisha kuwa ni mwanamitindo. Kwa kitendo cha kusema ni mwanamitindo wakati huko mitandaoni sifa (reputation) yake ni kuweka picha za utupu, kuweka picha za mapozi ya hovyo ni kuharibu taswira ya sekta ya mitindo Tanzania.

Kwa kujitambulisha kwake ni mwanamitindo maana yake, matendo yake ya ovyo yatahukumiwa kama matendo ya wanamitindo. Na kwa kuwa ni kawaida kwa jamii kuhukumu mambo kwa ujumla, basi ujinga wa Sanchi utakuwa ujinga wa wanamitindo.

Watu wamitindo wako wapi kusema juu ya tabia za huyu binti?

Kama kweli Sanchi ni mwanamitindo kama yeye anavyopenda kutambulika, basi wakuu wa sekta hiyo wanabidi wakae naye chini na kumpa somo. Kuacha Sanchi kuendelea kuposti picha zake za utupu, kuongea ovyo ni hatari kwa sekta ya mitindo.

Ili sekta yoyote ikue huwa inahitaji damu changa na taswira njema kwa jamii. Sasa ni kwa vipi wazazi watawaruhusu watoto wao kuingia katika sekta hiyo kama inaonekana ni  sekta ya kina Sanchoka waweka picha za utupu katika mitandao?

Katika jamii ya kitanzania, binti wa kike kukaa utupu hadharani ni matusi kwake, familia yake na kwa watu wazima wote. Mzazi gani ataruhusu binti yake apate laana ya kuwakosea heshima watu wazima wote? Hiyo ni katika mrengo mmoja.

Mrengo mwingine ni kwamba kama Sanchi siyo mwanamitindo kama anavyosema. Maana yake ni kuwa anatumia jina la fani hilo kujikinga kwa ujinga anaofanya. Kama iko hivyo, wakuu wa sekta ya mitindo wako wapi kumkanusha na kusema yeye ana ‘mambo’ yake na siyo mwanamitindo kama anavyodai na alikome kujiita mwanamitindo?

Kumuacha Sanchi aendelee na kuweka picha zake za utupu kabisa huku akitumia jina la uanamitindo ni hatari.

Kabla ya sekta ya mitindo kukubaliwa, imewahi kupita katika vipindi vigumu mno.

Wazazi na wana jamii wengi walikuwa ni wagumu kutofautisha sekta hiyo na uhuni. Kazi kubwa ilibidi kufanyika, bidii kubwa ilibidi kutumika na elimu kubwa ikalazimu itumike hatimaye jamii ikaelewa. Kwa kazi kubwa ya namna hiyo.

Kwa muhanga mkubwa wa kuelemisha uliofanyika, wadau wanaacha vipi mtu mmoja, anayeitwa Sanchi aharibu taswira njema iliyojengwa kwa  muda mrefu na kwa gharama kubwa?

Sanchi anatukanisha wanamitindo. Sanchoka anaharibu jina zuri la fani ya mitindo. Kwa heshima ya fani hii, inabidi Sanchi aambiwe abadilike ama akanushe kusema yeye siyo mwanamitindo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles