27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

ZIFF, WANENE WAWASHINDANISHA RAYVANNY, JUX, DARASA

Na FESTO POLEA,

TAMASHA la 20 la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF) kwa kushirikiana na Kampuni inayojishughulisha na uandaaji wa video na filamu za wasanii mbalimbali nchini, Wanene Entertainment watawashindanisha wasanii wa Tanzania, Kenya na Uganda kwenye kipengele cha video bora ya muziki Afrika Mashariki.

Mshindi katika kipengele hicho atarekodiwa bure video ya wimbo wake atakaotaka na Kampuni ya Wanene kwa gharama zote na video hiyo itafanyika sehemu mbalimbali za Tanzania, lengo likiwa ni kutangaza utalii wa ndani na kuvutia wasanii wa nje kuja kutumia mandhari za Tanzania.

Mkurugenzi wa Masoko Ziff, Isihaka Mlawa, alitaja vigezo vya video hizo ni kwamba zinatakiwa ziwe zimetengenezwa ndani ya ardhi ya Afrika Mashariki na mwongozaji wake awe ametoka kwenye nchi hizo, lakini ukitengenezwa Afrika Mashariki na mwongozaji akatoka nje ya nchi hizo video inakuwa imekosa vigezo.

Mlawa alizitaja video zikazoshindanishwa ni ‘Natafuta Kiki’ wa Rayvvany, ‘Umenikamata’ wa Jux na ‘Muziki’ wa Darasa aliomshirikisha Ben Pol kwa Uganda ni ‘Jubilation’ wa Eddy Kenzo, ‘Nkwatako’ wa Sheebah Karungi na ‘A Pass’ wa Gamululu kutoka Kenya zinazoshindanishwa ni ‘Everlast’ wa Gudi Gudi, ‘Uko’ wa Avril na ‘Problem’ wa Nai boi.

Naye Mkurugenzi wa Wanene Entertainment, Darsh Pandit, alisema watadhamini kila kitu kuanzia uandishi wa muswada wa video hiyo na upangaji wa mandhari zote za video hizo kwa kiwango cha juu, lengo likiwa ni kutangaza utalii wa ndani na kukuza mandhari za Tanzania nje ya nchi.

“Tunafanya hivi ili kukuza utalii lakini kushawishi wasanii wengine wa nje waje Tanzania kufanyia video zao kwa kuwa tunaamini kuna maeneo mazuri hapa nchini kwetu, lakini hayatumiki kwenye video za wasanii wetu, sisi tunataka tuwe wa kwanza kuonyesha kupitia mshindi atakayepatikana,” alisema Darsh.

Tuzo hiyo kwa mara ya kwanza ilitolewa kwenye tamasha la 29 la Ziff na ilichukuliwa na rapa, Fareed Kubanda (Fid Q) kupitia video ya wimbo wake wa ‘Walk it off’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles