25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

LIKIZO YA HAKIMU YAKWAMISHA KESI INAYOMKABILI ‘SCORPION’

Salum Njetwe maarufu ‘Scorpion’

Na FARAJA MASINDE-DAR ES SALAAM

KESI ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi, inayomkabili Salum Njetwe maarufu ‘Scorpion’, imeshindwa kuendelea kusikilizwa kwa mara ya saba mfululizo baada ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo kuwa likizo.

Kesi hiyo iliahirishwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassani kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali, Adolf Kisima hadi Julai 18, mwaka huu.

Hatua hiyo ilitokana na Hakimu Mkazi Flora Haule anayesikiliza shauri hilo kuwa likizo.

Hadi sasa mashahidi wanane wa upande wa mashtaka wamekwisha kutoa ushahidi wao dhidi ya mtuhumiwa ‘Scorpion’ anayekabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Juni 20, mwaka huu, kesi hiyo ilishindwa kuendelea baada ya magereza kushindwa kumleta mahakamani mtuhumiwa huyo.

Juni 8, mwaka huu, kesi hiyo pia ilishindwa kuendelea kusikilizwa baada ya Hakimu   Flora Haule kuwa mgonjwa.

Mei 25, mwaka huu, kesi hiyo pia ilishindwa kuendelea kutokana nawakili wa utetezi, Juma Nassoro kushindwa kufika mahakamani.

Katika awamu nyingine, Mei 15, mwaka huu, kesi hiyo ilikwama tena   kusikilizwa baada ya upande wa mashtaka kutokuwa na shahidi.

Mei 2 mwaka huu kesi hiyo iliahirishwa kwa mara nyingine baada ya shahidi namba nane kwenye kesi hiyo ambaye alitakiwa kuulizwa maswali na wakili wa utetezi, kuwa mgonjwa kwa mara ya pili.

Pia Aprili 18, mwaka huu, kesi hiyo ilishindwa kuendelea baada ya shahidi kuwa mgonjwa na kushindwa kufika mahakamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles