28.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 18, 2024

Contact us: [email protected]

MAPACHA WA JAY Z WANAVYOWAUMIZA KANYE, KIM

NEW YORK, MAREKANI



SIKU chache baada ya rapa, Jay Z na mke wake Beyonce kufanikiwa kupata watoto mapacha wawili na kufikisha idadi ya watoto watatu, msanii mwenzake Kanye West na mke wake, Kim Kardashian, wapo mbioni kukodi mwanamke wa kubeba ujauzito wao ili nao wapate mtoto wa tatu kama wao.

Kinachosababisha wawili hao wasake mwanamke wa kuwabebea ujauzito huo, kinatokana na ushauri aliopewa Kim Kardashian na madaktari kutokana na tatizo la uzazi linalomsumbua.

Kanye West na Kim wameweka wazi kwamba mwanamke aliye tayari kubeba mimba yao atapewa zaidi ya milioni 247 na endapo watoto watakuwa mapacha, mwanamke huyo atapewa zadi ya bilioni 2, huku kila mtoto akiwa na thamani ya zaidi ya bilioni 1.

Wawili hao wameongeza kwamba endapo itatokea bahati mbaya mama huyo akapata tatizo la kizazi baada ya kujifungua, atapewa fedha zaidi ya milioni 8.

Hata hivyo, inadaiwa kwamba mdogo wa Kim alikuwa tayari kubeba ujauzito huo, lakini baada ya wataalamu kumpima amegundulika kuwa ana tatizo la kizazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles