25.4 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

MAJALIWA: MAOFISA MIFUGO BADILIKENI

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa

Na MWANDISHI WETU,

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amewataka maofisa mifugo wa wilaya na mikoa kote nchini kubadilika ili sekta hiyo iweze kuongeza mchango wake kwenye pato la Taifa.

Majaliwa alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na maofisa mifugo kutoka wilaya na mikoa yote wanaohudhuria kikao alichokiitisha ili kujadili namna wanavyoweza kubadili uchungaji kuwa ufugaji mjini Dodoma.

“Katika ziara zangu za mikoani nimekuwa nikionesha kutoridhishwa kwangu na utendaji kazi wenu na hasa jinsi tunavyoendesha ufugaji hapa nchini. Mmeacha kazi ya kuwaongoza wafugaji, wanafanya wanavyotaka, tunahitaji kuona mabadiliko makubwa katika sekta hii,” alisema.

Alisema takwimu za mwaka 2016 zinaonyesha Tanzania ni nchi ya tatu barani Afrika na ya 11 duniani kwa ufugaji, ikiwa na ng’ombe takriban milioni 24, nyuma ya Ethiopia yenye ng’ombe milioni 54 na Sudan yenye ng’ombe 41.

“Wakati sekta ya mifugo inatoa mchango usiozidi asilimia 10 kwenye pato la Taifa, wenzetu Ethiopia sekta hiyo hiyo inachangia asilimia 14 kwenye pato lake na asilimia 16 ya fedha za kigeni.

“Nchi kama Botswana na Namibia, nazo zinafanya vizuri kwenye sekta ya mifugo, pamoja na kwamba wana mifugo michache na eneo dogo la ardhi,” alisema na kuongeza:

“Ni lazima tuanze kufikiri tofauti na kujitathimini kama kweli tunawatendea haki Watanzania waliogharimia elimu yetu na wanaoendelea kutulipa mishahara.

“Ningependa kupata ufahamu wenu wa kitaalam mna mipango gani kuinua sekta hii kwa kuwafanya wafugaji wa Tanzania wawe wafugaji wanaotumia utaalam na hatimaye wao wenyewe na Taifa zima linufaike kwa kupunguza umaskini,” alisisitiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles