19.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

BOT YAONYA WANAOCHEZA ‘DECI YA MTANDAONI’

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango

MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

BENKI  Kuu ya Tanzania (BoT) na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), zimewaonya wananchi wanaocheza upatu wa taasisi ya D9 Club kwa njia ya mtandao na kusema kuwa watapoteza fedha zao.

Maelfu ya Watanzania wamejiunga kwenye mchezo huo unaochezwa kwa njia ya mtandao, ambapo baadhi yao wamekopa fedha benki na kuweka kwenye taasisi hiyo kwa matumaini ya kupata faida mara dufu.

Hivi karibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, aliliambia gazeti hili kuwa kwa sasa hawezi kuzungumza chochote hadi bajeti yake itakapopita.

Baada ya kutoka kwa taarifa hiyo, BoT na CMSA wametoa taarifa ikisema, D9 Club inashawishi watu kununua hisa bila vibali vya mamlaka husika.

“Ni imani ya BoT na CMSA kuwa ushawishi unaofanywa na D9 Club kwa umma kushiriki katika mpango wao utasababisha watu kupoteza fedha zao.

“Pia ni kinyume na Sheria ya Makosa ya Jinai Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania ambayo katika Fungu la 171A,171B na 171C, ni kosa la jinai kuendesha, kushawishi watu kushiriki, na kushiriki au kuchangia fedha katika upatu.

“Ifahamike kwamba upatu haramu hubuniwa kwa namna ambayo fedha za kila mshiriki mpya hutumika kumlipa mshiriki aliyetangulia, na hakuna maelezo ya namna yoyote ya kuwekeza au kuzalisha fedha hizo.

“Kwa taarifa hii, umma unasisitizwa kutoshawishika kwa namna yoyote ile kushiriki katika upatu uliobuniwa na D9 Club na mipango mingine ya aina hiyo.

“Wananchi watoe taarifa kwa vyombo vinavyohusika, ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana na vyombo vya usalama (Polisi) kuhusiana na mikutano au mafunzo yanayoendeshwa na D9 Club na mipango mingine haramu kama inayofanana na huo,”inasema sehemu ya taarifa hiyo.

“D9 CLUB au D9 SPORT Trading kama inavyojulikana na wengi ni biashara ya kuuza na kununua hisa za michezo ya kimataifa ambapo mwanachama anapata faida kila wiki kulingana na hisa zake kwenye kampuni.

“Kwa wanaocheza mchezo huo, wanasema faida kwa kampuni hupatikana kutokana na wataalamu wa kubashiri matokeo ya michezo ya kimataifa ambapo anayenunua hisa, yeye hupata faida hiyo bila kubashiri moja kwa moja michezo hiyo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,660FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles