25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

WANAONAWISHA WATU MIGUU, KUWAVUSHA WAONYWA

Mwendesha Bodaboda akimvusha abiria wake kwenye dimbwi la maji katika Barabara ya Ubungo Maziwa yaliyosabishwa na mvua zinazoendelea, Dar es salaam jana. PICHA : IMANI NATHANIEL.

 

 

HAPPY MOYO (RCT) Na TUNU NASSOR, DAR ES SALAAM

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ubungo,  imewaonya watu wanaojihusisha na shughuli za kuosha watu miguu maeneo ya sokoni kuwa ni kinyume cha sheria na si salama kwa afya.

Mbali na hilo pia wanaofanyabiashara ya kubeba watu mgongoni ili kuwavusha katika matope na maji kuwavusha kutoka eneo moja kwenda jingine kutokana na sababu za kiafya kama ilivyotajwa hapo juu.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya kuwapo na mwanamke, Sarafina Mohamed katika soko la Mabibo maarufu ‘mahakama ya ndizi’ kubuni kazi ya kuosha miguu iliyojaa matope wateja wanaotoka sokoni hapo kwa ujira wa kati ya Sh 100 na 500.

Imezoeleka katika jiji la Dar es salaam na mikoa jirani vija wasiokuwa na ajira kutumia  fursa hiyo kuvusha watu katika madimbwi ya maji au madaraja mabovu kwa kuwabeba mgongoni kwa ujira kati ya Sh 200 hadi 1000 kutegemea na eneo husika.

Akizungumza na MTANZANIA jana ofisini kwake, Ofisa Afya wa Manispaa hiyo, Allan Kalongola alisema ni kinyume cha sheria namba moja ya mwaka 2009 ya afya ya jamii ambayo hairuhusu kufanya kazi hiyo bila kibali.

“Hiki kinachofanyika hakiruhusiwi kisheria na kiafya pia si salama kwao na wateja wao pia,” alisema Kalongola.

Alisema ili mtu aweze kutoa huduma kwa wengine lazima awe amepimwa afya yake na kupatiwa kibali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles