29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

WABUNGE CUF MBARONI KWA TUHUMA ZA MAUAJI

\

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

WAKATI Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF), likitoa maazimio yake ikiwemo kubariki kuvuliwa kufurushwa kwa kuvuliwa uanachama vigogo wake, wabunge wawili wa chama hicho wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani kwa tuhuma za kutishia kumuua mbunge mwenzao.

Akizungumza na MTANZANIA jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,  Lazarto Mambosasa, alisema kuwa wabunge hao wamehojiwa kutokana na tuhuma za kudaiwa kumtishia kumuua Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya (CUF).

Viongozi hao wa CUF  wamekuwa na mvutano ndani ya chama kwa muda mrefu sasa na kupelekea kuzaliwa kwa makundi mawili likiwemo linalomuunga mkono Mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama, Profesa Ibrahim Lipumba na lile linalomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.

Kamanda Mambosasa, alisema baada ya mahojiano na wabunge hao jeshi hilo liliwaachia huru ili waweze kuendelea na majukumu yao na kutakiwa kufika polisi pale watakapohitajika.

“Ni kweli tumewahoji sababu kubwa ni kumtishia kumuua Mbunge mwenzao Sakaya ila tumewahoji tu na kuwaachia waendelee na shughuli zao,’’ alisema

Akizungumzia Sakata hilo, nje ya Kituo cha Polisi, Katibu wa wabunge wa CUF,  Juma Kombo Hamad, ambaye pia ni Mbunge wa Wingwi, alisema wabunge hao walikamatwa kutokana na taarifa zilizotolewa na Sakaya kuhusu kutishiwa maisha ambapo alisema hayo ni masuala la kisiasa.

“Haya ni mambo ya kisiasa tu yakataa vizuri na maisha yataendelea,’’ alisema Juma

Jana Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF, Julius Mtatiro alitangaza maazimio la kikao cha Baraza Kuu laUongozi lililoketi Visiwani Zanzibar ambapo kikao hicho kilibariki kuvuliwa uanachama kwa vigogo wake saba ambao, ni  Mohamed Habibu Mnyaa, Haroub Shamis, Mussa Haji Kombo, Khalifa Suleiman Khalifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles