27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

MAT WAIGOMEA SERIKALI KUPELEKA MADAKTARI KENYA

Mmoja wa madaktari ambao walihiriki mgomo, wakiandamana hivi karibuni jijini Nairobi.

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

CHAMA cha Madaktari Tanzania (MAT), kimepinga uamuzi wa serikali kuipatia Kenya madaktari 500 na kuiomba isimamishe mara moja uamuzi wake huo.

MAT imesisitiza serikali isiipatie Kenya madaktari wake hadi   nchi hiyo itakapoanza utekelezaji wa makubaliano kati yake na madaktari wao ambao waligoma kwa karibu miezi mitatu hivi karibuni.

Machi 18, mwaka huu serikali ilitangaza kuwa imeridhia madaktari wake 500 kuajiriwa na serikali ya Kenya baada ya kupokea ombi kutoka kwa Rais   Uhuru Kenyata.

Akizungumza na waandishi wa habari   Dar es Salaam jana, Rais wa MAT, Dk. Obadia Nyogole, alisema uamuzi wa Serikali umezua mitazamo tofauti baina ya madaktari wa Kenya na wa Tanzania.

“MAT tulipata taarifa kupitia vyombo vya habari kwamba serikali imeridhia ombi hilo la Kenya, na tumeona barua katika mitandao ya jamii kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubsya ambayo inatoa maelekezo ya maombi ya kazi kwa madaktari wanaohitaji.

“Hivyo ni muhimu kujua kwamba jambo hili nyeti limefanyika bila MAT kushirikishwa katika hatua yoyote, lakini baada ya taarifa hiyo kutolewa ni jukumu letu la taaluma kutoa ushauri, maoni na mapendekezo kujenga ustawi bora wa udugu wa wanataaluma ndani na nje ya nchi,” alisema Dk. Nyogole

Alisema   ripoti ya TSPGHSST (Task Sharing Policy Guidilines for Health Sectors in Tanzania) ya mwaka 2016, inataja sekta ya afya nchini kuwa na upungufu mkubwa wa wataalamu wa afya wapatao 2,430 au asilimia 75.

Akitoa mfano, alisema  katika vituo vya afya mahitaji ni madaktari 771 wakati waliopo ni 57 pekee, katika hospitali za wilaya mahitaji ni madaktari 1,760 lakini waliopo ni 441, katika hospitali za mikoa mahitaji ni 725 lakini waliopo ni 328.

“Kwa maana hiyo Tanzania inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madaktari pengine kuliko Kenya na tufahamu kwamba Chama cha Madaktari Kenya kupitia katibu wake, Dk. Ouma Oluga kimesema kuna madaktari 1,400 ambao hawajaajiriwa.

“Yamekuwapo maoni tofauti juu ya madaktari wa Tanzania kwenda  Kenya  na zaidi ya asilimia 60 ya madaktari wa nchi hiyo wamepinga suala hilo na kutaka waajiriwe  wazawa kwanza.

“…kuna maoni tofauti pia nchini baadhi ya madaktari wanaunga mkono na wengine wanapinga.  MAT kwa kuwa hatukushirikishwa  tunayo maswali haya kwa serikali. "alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles