32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Waganga 13 wa jadi watiwa mbaroni Katavi

NA WALTER MGULUCHUMA, KATAVI
JESHI la Polisi Mkoa wa Katavi, limewakamata waganga 13 wa jadi katika Tarafa ya Mamba, Wilaya ya Mlele, kwakudaiwa kufanya kazi hiyo bila vibali maalumu.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba, waganga hao walikamatwa baada ya msako uliofanyika Machi 14 na 15 mwaka huu.
Pamoja na waganga hao kukamatwa, pia walipopekuliwa kwenye nyumba zao walikutwa na vitu mbalimbali wanavyovitumia kufanyia shughuli hizo.
Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Sudi Ngereja (46), Charles Kamanija (78), Peter Mnulu (66), Benedicto Hilali (53), Fuso Tungu (37), Gamaweshi Nkobe (65) na Isuha Mwakayandogi (35).
Wengine ni Sukari Rusinge (38), Sila Halawa (30), Nyembe Makoye (38), Suzana Marko (70), Nyalida Jilangaida (43) na Maraika Paulo (44) wote wakazi wa Kata ya Maji Moto, Wilaya ya Mlele.
“Wakati wa msako huo, watuhumiwa wanne walikamatwa wakifanya kazi ya uganga jambo ambalo hatuwezi kuendelea kulivumilia,” alisema Kamanda Kidavashari.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, watuhumiwa waliokuwa hawana vibali vya kazi hiyo watafikishwa mahakamani baada ya taratibu zote kukamilika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles