NA CHRISTOPHER MSEKENA
KIPAJI kinaweza kukufanya uibuke shujaa mbele ya wenzako baada ya kuwaokoa kufuatia kuandamwa na adhabu kali. Ushujaa huo ulimkuta mchekeshaji mahiri nchini aliyejizolea umaarufu kwa kuiga sauti za watu mashuhuri, Shafii Omari ‘JK Comedian’ baada ya kuokoa wapiga kelele.
Akizungumza na Juma3tata, Jk Comedian alisema kuwa wakati ana soma sekondari shule ya Southern Highland jijini Mbeya amewahi kuokoa darasa zima lililokuwa linakabiliwa na adhabu ya kuchapwa bakora kwa kosa la kupiga kelele.
“Mimi ndiyo nikawa mkombozi wao, niliweza kuigiza sauti ya Naibu Waziri wa Elimu kwa wakati huo Mh Philipo Mulugo, kitu ambacho kilifanya nijizolee ujiko kwa wanafunzi wenzangu,” alisema Jk.
Aliongeza kuwa alifanikiwa kuvunja mbavu za walimu mpaka wanafunzi wenzake, tukio lililofanya darasa zima kusamehewe adhabu ya viboko nay eye kuwa maarufu shuleni hapo.