30.8 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

WALIOKAMATWA POLISI WAFIKIA 112

Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM

IDADI ya watu wanaotuhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya katika Jiji la Dar es Salaam imefikia 112.

Kati ya watuhumiwa hao, 12 watawekwa chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi na mahakama kwa muda wa miaka miwili, wakitakiwa kuotenda kosa na pia watatakiwa kuripoti polisi mara mbili kwa mwezi.

Wiki iliyopita baadhi ya wasanii na wafanyabiashara walianza kuripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam (Central) baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kuwataja kuhusika na biashara hiyo.

Wasanii walioripoti jana ni Khalid Ramadhani ‘Tunda Man’ ambaye alifika kituoni hapo saa 1 asubuhi na Rachel Haule ‘Recho Kizunguzungu’ aliyefika saa 3:58.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, alisema baadhi yao walipohojiwa walikiri kutumia na kuwataja watu wanaowauzia na wengine kwenda mbali zaidi kwa kutaja dawa wanazozipenda.

“Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) iko wazi, kifungu cha 73 na 74 huwa tunaweza kuomba kwa hakimu tukiwaombea watuhumiwa wabadilishe tabia zao, wawe chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi na mahakama kwa muda wa miaka miwili wasifanye makosa.

“Hata hao wanaosema wana ‘brand’ kubwa wamejitahidi kutoa ushirikiano na wako waliokamatwa na vielelezo, wengine wamekiri kutumia na wametusaidia sana kwenda kuwakamata wanaouza. Nimejitahidi mwenyewe kuwahoji mmoja mmoja, niliona kuwapa wapelelezi wawahoji wanaweza wasitende haki… mimi ni kachero mzoefu,” alisema Sirro.

Aliwataja watuhumiwa watakaowekwa chini ya uangalizi kuwa ni Wema Sepetu, Khalid Mohamed maarufu kama TID, Omar Michen, Hamidu Chambuso ‘Dogo Hamidu’, Rajabu Salum, Romeo George, Sideo Bandigo, Johanes Maisen, Lulu Shelangwa, Ahmed Hashim ‘Petit Man’, Said Masoud ‘Alteza’, Nassoro Mohamed na Bakari Khelef.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles