32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

OBAMA AWAAGA WAMAREKANI KWA HOTUBA NZITO

Rais wa Marekani, Barack Obama (kulia), mkewe Michelle, mtoto wao Malia, Makamu wa Rais Joel Biden na mkewe Jill wakiaga baada ya Obama kutoa hotuba ya mwisho kama Rais mjini Chicago juzi.
Rais wa Marekani, Barack Obama (kulia), mkewe Michelle, mtoto wao Malia, Makamu wa Rais Joel Biden na mkewe Jill wakiaga baada ya Obama kutoa hotuba ya mwisho kama Rais mjini Chicago juzi.

CHICAGO, MAREKANI

RAIS Barack Obama, amewaaga Wamarekani na ulimwengu mzima kwa hotuba iliyojaa hisia, aliyoitoa mjini hapa na kuwataka Wamarekani kuunganisha nguvu katika kuleta mabadiliko.

Mbele ya wafuasi wake 18,000, Rais huyo alitokwa na machozi wakati akimshukuru mke wake Michelle Obama kwa namna alivyotoa mchango mkubwa katika utawala wake.

Akihitimisha utawala wake katika Ikulu ya Marekani, Obama amerejea Chicago, mji ambao ni nyumbani kwake, ambako kampeni yake ya ‘ndio tunaweza’ ilianzia hapo na jana alisema ‘ndio tumeweza’.

Katika hotuba hiyo Rais Oboma aliorodhesha mafanikio ya utawala wake wa miaka minane kuanzia mkataba wa nyukilia na Iran hadi huduma ya bima ya afya.

Hata hivyo, sehemu kubwa ya hotuba yake iliegemea katika kuwatia moyo wafuasi wake walioshtushwa na ushindi wa Donald Trump pamoja na kutathmini mafanikio aliyoyapata katika uongozi wake na mtazamo wake kuhusu wapi Marekani inaelekea .

Obama amewataka Wamarekani kuamka, kupigania demokrasia lakini akaonya kuwa ubaguzi wa rangi na kukosekana kwa usawa bado ni kitisho kwa demokrasia.

“Sisi sote bila ya kujali vyama, ni lazima turudi katika ujenzi wa taasisi ya demokrasia.

“Hivyo sisi kama wananchi, lazima tuwe macho dhidi ya uchokozi wa nje, ni lazima tuilinde misingi yetu inayodhoofika inayotutambulisha sisi ni akina nani.

“Ndio maana katika kipindi cha miaka nane iliyopita nimefanya kazi ya kuweka mapambano dhidi ya ugaidi katika misingi ya kisheria.

“Ndio maana tumemaliza mateso, kufanya kazi kulifunga Gereza la Guantanamo na mageuzi ya sheria zetu zinazosimamia ufuatiliaji wa kulinda faragha na uhuru wa raia. Na ndio maana mimi nimekataa ubaguzi dhidi ya Waislamu Wamarekani,” amenukuliwa rais huyo.

Mke wake Michele Obama na Makamu wa Rais, Joe Biden na mke wake Jill ambao rais aliwaelezea kama ‘familia’ na kuwamwagia sifa walihudhuria hafla hiyo.

Huku akifuta machozi, Obama alimshukuru mke wake Michelle aliyemuita rafiki yake na kuwasifu watoto wake Malia na Sasha, ambaye alibubujikwa machozi. Malia hakuwepo.

Obama katika hotuba yake ya mwisho, ambayo pia ilimtoa machozi Biden, aliepuka kumkosoa Trump moja kwa moja na kulaani mgawanyiko ambao umezikumba siasa za taifa hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles