27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

MAJALIWA AITAKA TAN COAL KUANZA KUZALISHA UMEME

 WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa

Na Mwandishi Maalumu – Ruvuma

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, ameitaka Kampuni ya Tan Coal Energy inayochimba makaa ya mawe katika mgodi wa Ngaka itimize masharti ya mkataba iliouingia na Serikali mwaka 2008.

Kampuni hiyo iliundwa Aprili 3, 2008 na Kampuni tanzu ya Atomic Resources Limited ambayo wakati huo ilikuwa ikijulikana kama Pacific Corporation East Africa (PCEA). Kwa sasa inaitwa Intra Energy (T) Limited ikiwa na hisa asilimia 70 na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) asilimia 30.

Akizungumza mjini hapa jana baada ya kutembelea mgodi huo na kukagua shughuli za uzalishaji, alisema kwa mujibu wa mkataba huo, ilikubaliwa kwamba mbali ya kuzalisha makaa ya mawe, kampuni hiyo ilipaswa kuzalisha umeme wa megawati 400 kutokana na makaa hayo.

“Katika mkataba tulikubaliana kuwa mtazalisha umeme, lakini hadi leo hamjaanza mnadai kuwa Tanesco wanawachelewesha. Nitafuatilia nione kama ni wao au la ili tujue ukweli,” alisema Majaliwa.

Kwa mujibu wa mkataba huo, Tan Coal ilipaswa kugharamia dola milioni 14.49 za Marekani kwa ujenzi wa barabara na madaraja ili kuwezesha malori makubwa na madogo kufika mgodini na kusomba makaa hayo.

“Mlisema mngetengeneza barabara, lakini hadi sasa bado hamjafanya hivyo na ndiyo maana malori yanaishia kule. Yangefika hapa moja kwa moja, mngeweza kubaini kwa urahisi mahitaji ya makaa ya mawe ni kiasi gani,” alisema Majaliwa.

Hivi sasa malori ya kutoka mgodini yanashusha makaa yaliyochimbwa katika eneo lililokodishwa na Tan Coal la Amani Makolo, kilomita 55 kutoka mgodini na malori makubwa yanapakia makaa hayo kutoka eneo hilo jambo linalozidisha gharama za usafirishaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles