30 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

SADIFA: SITAGOMBEA UBUNGE 2020

MBUNGE wa Donge, Sadifa Juma Khamis
MBUNGE wa Donge, Sadifa Juma Khamis

Na Mwandishi Wetu – Zanzibar


MBUNGE wa Donge, Sadifa Juma Khamis, jana alitangaza kuwa hatagombea tena ubunge mwaka 2020, huku akimshutumu hadharani Katibu wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mulla Othman Zubeir, akidai anachochea mgawanyiko ndani ya chama.

Alisema hakuna mtu anayezaliwa na uongozi, bali uongozi ni matokeo yanayomkuta binadamu  katika mchakato wa maisha yake na hivyo si jambo la kudumu.

Sadifa alisema hayo akiwa Donge Vijibweni, Mkoa wa Kaskazini Unguja, kabla ya kuanza matembezi ya vijana wa CCM kuadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964.

Alisema kuwa ameamua kuliweka wazi suala hilo mbele ya Naibu Katibu Mkuu Bara, Rodrick Mpogolo aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa matembezi hayo na kuwataka wanaomwandama kwa majungu na chuki waache kumchimba.

“Kuna watu wananiandama usiku na mchana kwa sababu tu ya ubunge, sikuzaliwa na ubunge, ubunge ni matokeo, acheni kunisakama kwa sababu mwaka 2020 sitagombea tena,” alisema Sadifa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).

Aidha alidai kuwa Mulla ni kiongozi anayependelea upande mmoja na kuwalinda watu wakorofi kwa sababu zake binafsi, bila kujali masilahi ya chama na mshikamano.

Akizungumzia madai hayo, Mulla alisema kuwa alichokipinga yeye ni tabia ya ubabe wa Sadifa kumwamuru Katibu wa CCM wilayani, Subira Mohamed Ameir amwandikie barua ya kumsimamisha katibu wa chama hicho Jimbo la Donge, Haji Khamis Vuai ‘Boko’ kinyume na taratibu na Katiba ya CCM.

“Madai yake hayana msingi wala ukweli wowote, alitaka kuvunja kanuni na taratibu nikampinga, tumejadili katika kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa, maamuzi yakaonekana hana haki wala nguvu za kikatiba kumsimamisha kiongozi,” alisema Mulla.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles