28.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 18, 2024

Contact us: [email protected]

PLUIJM: NIPO TAYARI KUIFUNDISHA STARS WAKINIHITAJI

Na ADAM MKWEPU -DAR ES SALAAM


hansMKURUGENZI wa benchi la ufundi la timu ya Yanga, Hans van der Pluijm, amesema yupo tayari kuifundisha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, kama Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litamhitaji kufanya mazungumzo kuziba nafasi iliyoachwa wazi na kocha, Boniface Mkwasa.

Kauli hiyo ya Pluijm imekuja siku moja baada ya TFF kutangaza kuvunja mkataba na kocha mkuu wa timu hiyo, Mkwasa, huku nafasi yake ikichukuliwa kwa muda na kocha wa timu ya Mtibwa Sugar, Salum Mayanga.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Pluijm alisema licha ya kufungua milango kwa shirikisho hilo, zipo hatua za kuchukua katika mazungumzo hayo kwa kuwa bado ana mkataba na Yanga.

“Nipo tayari kufanya mazungumzo si na TFF pekee bali hata Azam kama watahitaji kufanya hivyo, lakini naheshimu mkataba wangu na Yanga hivyo wakija kwangu watatakiwa kulizingatia jambo hilo.

“Mbali na mambo yanayozungumzwa kuhusu mimi, hadi sasa si uongozi wa Azam wala TFF ulionifuata kufanya mazungumzo ili kuzifundisha timu zao,” alisema Pluijm.

Hata hivyo, Pluijm alisema kuifundisha timu ya taifa si suala rahisi, linahitaji kufanya uamuzi mkubwa kwani linaamua hatima ya maisha ya soka ya baadaye hivyo si jambo la mchezo.

“Kuifundisha timu ya taifa inahitaji umakini wa hali ya juu sana, hivyo kabla ya kuamua natakiwa kufikiri zaidi na ninafanya hivyo,” alisema Pluijm.

Hata hivyo, taarifa zinadai kuwa yapo mazungumzo ya siri kati ya kocha huyo na Azam, iwapo mazungumzo hayo yatafanikiwa huenda wakamtangaza kuifundisha Azam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles