MONTEVIDEO, Uruguay
MSHAMBULIAJI wa Liverpool na timu ya taifa ya Uruguay, Luis Suarez,
amemuomba radhi beki wa Italia na Juventus, Giorgio Chiellini, kwa kitendo chake cha kumng’ata begani wakati wa mchezo baina ya timu hizo.
Suarez aliyefungiwa kucheza soka miezi minne pamoja na kulipa faini ya pauni 65,000, amesema kuwa tukio hilo lilitokea baada ya kukosa nguvu hivyo ni ajali ya kawaida katika soka.
Mruguay huyo wa Liverpool huenda akauzwa kwa pauni milioni 80 baada ya klabu ya Barcelona kusisitiza kutaka kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 27.
Kwa mujibu wa mchezaji wa zamani wa Barcelona, Gary Lineker, amesema kuwa miamba hiyo ya Catalan imedhamiria kumsajili Luis Suarez, hivyo hatua ya kuomba radhi ni kuweka sawa mambo ya usajili wake.