32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

KASI YA 5G KUANZA KUTUMIKA 2020

5g-mobile-technology

Na FARAJA MASINDE,

KATIKA sekta ya mawasiliano ni kawaida kuwasikia wataalamu na wakati mwingine watu wa kawaida wakizungumzia kuhusu teknolojia ya 2G, 3G, 4G na 5G huku badhi yetu tukiwa hatufahamu hasa undani wa mifumo hii.

Kwa kawaida herufi G imekuwa ikisimama kama ‘Generation’, yaani kizazi fulani cha teknolojia ya mawasiliano kwa kuangazia zaidi uwezo wa data kwenye simu.

Hata hivyo, hakuna kipimo chochote kinachotumiwa kimataifa kuhusu kasi ya data ya simu.

Japo wengi wanakubaliana kuhusu baadhi ya sifa za teknolojia hizi.

Teknolojia ya 1G, au kizazi cha kwanza cha data ya simu, ilianza kutumiwa 1991.

Huku ile ya 2G ilianza pia kutumika katika kipindi hicho, ikiwa kama ndugu wa 1G.

Kwa 1G, ungeweza tu kupiga simu. Teknolojia ya 2G ambayo pia huitwa teknolojia ya SMS iliwezesha watu kutuma ujumbe mfupi.

Ungeweza pia kutuma ujumbe wenye picha, ambao uliitwa MMS (multimedia messaging service).

Pia simu za wakati huo zilikuwa na teknolojia ya GSM, GPRS, EDGE kama hizi zilizo hapa chini.

Kupiga simu kwa video kuliwezekana mwaka 2001, 3G na kasi yake ya data ya 2mbit/s (megabaiti 0.25 kila sekunde) ilianza kutumika wakati ambao simu za kwanza aina ya ‘Smartphone’ zilipoanza kuuzwa madukani.

Huduma yake ya mtandao haikuwa ya kasi lakini iliwezesha huduma ya mtandao kupatikana bila kutumia nyaya.

Watu waliweza kupiga simu za video, 2010 teknolojia ya 4G ikaanza kutumika.

Teknolojia hii ya kasi iliwezesha kuanza kupatikana kwa michezo mingi kwenye simu na ya kiwango cha juu, kwani kitu ambacho ungepakua mtandaoni kwa saa tano kwa teknolojia ya 3G sasa inaweza ikakuchukua dakika 8 pekee kwa teknolojia ya 4G.

Hata hivyo, changamoto ni kuwa kasi hii ya 4G bado haipatikani maeneo yote, hata katika mataifa yaliyoendelea.

Tayari kampuni mbalimbali za utafiti wa kasi ya intaneti ikiwamo ile ya 5G Innovetion Center kutoka Uingereza, ambao wanasema kuwa teknolojia hiyo inatarajiwa kufanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza ifikapo 2018 huku ikitarajiwa kusambaa duniani miaka miwili baadaye yaani 2020.

5G inaelezwa kuwa bora mara 65,000 zaidi ikilinganishwa na kasi ya sasa ya 4G.

Tume ya Mawasiliano ya Ulaya inakadiria kwamba kati ya mwaka 2020 na 2030, utaweza kupakua filamu moja ya HD ya saa moja kwa sekunde sita pekee.

0653045474

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles