27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

ARUSHA WAFURAHIA KOMPYUTA ZA BAYPORT

Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Mercy Mgongolwa (kushoto), akimkabidhi kompyuta Ofisa Utumishi wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Emelda Kisosi, kusaidia ufanisi wa kazi kama sehemu ya kujitolea kwa jamii. Kulia ni ofisa Tehama wa  almashauri ya wilaya hiyo, Edna Mwaipiana.
Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Mercy Mgongolwa (kushoto), akimkabidhi kompyuta Ofisa Utumishi wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Emelda Kisosi, kusaidia ufanisi wa kazi kama sehemu ya kujitolea kwa jamii. Kulia ni ofisa Tehama wa almashauri ya wilaya hiyo, Edna Mwaipiana.

Na Mwandishi Wetu- Arusha

HALMASHAURI ya Wilaya Arumeru, mkoani Arusha, imepokea kompyuta mbili zilizotolewa msaada na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, kama sehemu ya ushirikiano, kusaidia na kukuza ufanisi wa kazi kwa watumishi wa umma wilayani humo.

Kompyuta hizo zinatoka ikiwa ni siku chache baada ya Mkoa wa Morogoro nao kupokea msaada kama huo kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa umma.

Akizungumza katika makabidhiano hayo jana, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, alisema wamefikisha kompyuta mbili katika wilaya hiyo kama orodha ya mahitaji waliyopokea kutoka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Alisema anaamini kwa kufikisha kompyuta hizo, kutachangia ufanisi wa kikazi kwa kutumia vyema teknolojia ya kompyuta iliyokuja kupanua wigo wa utendaji bora wa kazi kwa Tanzania nzima kwa hali ya kupanga, kuratibu na kuhifadhi kumbukumbu muhimu za kiutendaji wakati wote.

“Huu ni mwendelezo mzuri wa ugawaji wa kompyuta 205 tulizonunua zenye thamani ya Sh milioni 500 na tayari kompyuta 125 zimefikishwa Makao Makuu ya Utumishi na wao kutuelekeza eneo na idadi ya ugawaji kwenye halmashauri za nchi yetu,” alisema.

Naye Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya Arumeru, Imelda Kisosi, aliwashukuru Bayport kwa kujitolea vifaa hivyo muhimu vitakavyowapatia urahisi watendaji hao kuchapa kazi kwa nguvu zote ili wilaya yao isonge mbele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles