25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

KARAFUU YA Z’BAR KUUZWA SOKO LA ULAYA

karafuu

Na MWANDISHI WETU-ZANZIBAR

SHIRIKA la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC), litapatiwa hati ya kuuza karafuu  hai kwenye soko la Ulaya baada ya kutiliana saini na Kampuni ya Ganefryd  ya Denmark, makubaliano ya kuimarisha kilimo hai cha mazao tofauti kwa kuanzia na kilimo cha karafuu.

Mkataba huo wa makubaliano ulisainiwa jana mjini Unguja ambapo ZSTC iliwakilishwa na Mkurugenzi Mwendeshaji, Dk. Said Seif na Kampuni ya Genefryd iliwakilishwa na Ofisa wake, Pale Christeusen.

Akizungumza baada ya kutia saini makubaliano hayo, Dk. Said alisema Zanzibar imekuwa ikifanya biashara ya karafuu kwa miaka mingi lakini hivi sasa itapanua wigo wa kuuza karafuu hai Ulaya na kupata faida kubwa.

Alisema ili Zanzibar iweze kutoa karafuu hai tahadhari kubwa inapaswa kuchukuliwa wakati wa kuotesha miche, ukuwaji wake na kufikia wakati wa kuzaa bila ya kuingizwa aina yoyote ya mbolea zenye kemikali.

“Uangalizi mkubwa unahitajika katika mchakato mzima wa kushughulikia kilimo hicho kuanzia hatua ya kuchuma, kuanika, kuzihifadhi mpaka kuzisafirisha hivyo tunawaomba wananchi waunge mkono kwa kuingia kwenye kilimo hai kwa vile karafuu ndiyo tegemeo lao na Taifa kwa ujumla.

“Kuanzisha kilimo hai cha zao la karafuu  kutaongeza upandaji miche. Hivyo ni lazima tuache tabia ya kukata mikarafuu kwa ajili ya kuni, kufanyia mkaa na kujengea,” alisema Dk. Said.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles