29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Ukawa: CCM wanataka Katiba mpya itumike uchaguzi mkuu

Fredy Azzah, Dar es Salaam
UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umedai kubaini mpango wa siri wa Serikali kutaka kuipitisha kwa hila Katiba Inayopendekezwa itumike kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Hayo yalibainishwa jana na Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Freeman Mbowe, alipozungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama cha Wananchi (CUF) Buguruni, Dar es Salaam.
“Tumepata taarifa kuwa CCM imeamua aidha inyeshe mvua au isinyeshe, Katiba Inayopendekezwa itapita kwenye kura ya maoni waweze kuutumia kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.
“Tunamuomba Rais Kikwete amalize muda wake wa miaka 10, aondoke atuachie nchi yetu ikiwa salama kwa sababu mbinu hizo zinazoandaliwa zinahatarisha amani ya nchi,” alisema Mbowe.
Alisema wamepata taarifa kwamba baadhi ya sheria zimeanza kufanyiwa marekebisho lengo likiwa ni kuhakikisha Katiba hiyo inapita na kutumika kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Akitoa mfano, alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekuwa ikitumiwa kutoa matamko ambayo wakati mwingine hayana ukweli wowote.
“NEC wanasema siyo lazima kupitia na kuhakiki Daftari la Kudumu la Wapiga kura baada ya kuandikishwa, suala hili siyo uamuzi wao ni sheria inayowataka lipitiwe baada ya kuandikwa,” alisema Mbowe.
Alisema katika kile kinachoonyesha serikali inafanya kila njia kuharakisha Katiba hiyo, uandikishaji wa wapiga kura kwa mfumo wa BVR umejaa kasoro lukuki lakini serikali haitaki kukiri ukweli huo.
“Mathalani mashine za uadikishaji awali mahitaji halisi yalikuwa 8,000 lakini wakapata 250, taarifa nilizozipata leo kutoka Njombe ni mashine 80 tu ndizo zilizopo kwa madai kuwa nyingine zimepelekwa kwenye mikoa mingine kutoa mafunzo,” alisema.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva, wakati wa uzinduzi wa uandikishaji wapiga kura Njombe, alimweleza waziri mkuu kuwa wameweza kuandikisha wapiga kura 3,014 katika vituo 55.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles