Wabunge wa CORD nchini Kenya wamemgomea Spika wa Bunge hilo Justin Muturi kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge kuendesha kikao cha Bunge kilichoitishwa kwa dharura kurekebisha sheria ya uchaguzi iruhusu kura kuhesabiwa kawaida badala ya njia ya kielektroniki..
Katika mgomo huo, CORD wanataka utaratibu wa ‘electronic’ uendelee, walimtusi pia Rais Uhuru Kenyatta kwa madai kuwa ni njama za JUBIELEE kutaka kuiba kura katika uchaguzi wa mwakani
Hata hivyo JUBILEE wao wanataka sheria ibadilishwe ili tume ya uchaguzi itumie njia ya kawaida kuhesabu kura na hii ni kwa madai kwamba CORD wanataka kuiba kura kwa kutumia njia za kielektronik katika uchaguzi ujao.