WAJUMBE WAAMUA HATIMA YA URAIS WA TRUMP

0
490

WASHINGTON, MAREKANI


donald-trumpWAJUMBE wa Jopo la Kumchagua Rais nchini Marekani jana walianza utaratibu wa kuthibitisha matokeo ya uchaguzi wa urais nchini hapa, ambayo hata hivyo yatajulikana Januari 6 mwakani.

Katika uchaguzi wa awali, mshindi wa kura nyingi kwa kawaida alikuwa ndiye anapata kura nyingi za wajumbe, na hatua ya kumwidhinisha ilikuwa tu ya kutimiza wajibu.

Lakini safari hii, Rais mteule Donald Trump wa Chama cha Republican, alishinda kwa kupata kura nyingi za wajumbe kutoka kwa majimbo yaliyokuwa yanashindaniwa.

Mpinzani wake, Hillary Clinton, ambaye alikubali kushindwa, alipata kura nyingi za kawaida, akimzidi Trump kwa zaidi ya kura milioni mbili na nusu.

Hilo limezua mjadala mpya kuhusu mchango wa Jopo la Kumchagua Rais ambalo kwa Kiingereza hufahamika kama Electoral College.

Watu karibu milioni tano wametia saini ombi la kuwataka wajumbe kwenda kinyume na utamaduni na kumpigia kura Hillary.

Rais mpya ataapishwa mjini Washington Januari 20.

Mara ya mwisho mgombea kushindwa kwa kura nyingi za kawaida, lakini akakosa kuibuka mshindi wa urais ni mwaka 2000 wakati George Bush aliposhindwa na Al Gore kwa kura 500,000 lakini akafanikiwa kuingia Ikulu.

Katika mchakato wa jana, iwapo mgombea urais hatapata wingi wa kura za wajumbe (270), basi wabunge wa Bunge la Wawakilishi ndio huamua.

Kwa sasa Bunge hilo lina wabunge 435. Chama chenye wabunge wengi, ambacho baada ya uchaguzi kufanyika ni Republican, bila shaka kitamchagua mgombea wake, huku makamu wa rais akichaguliwa na Seneti.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here