29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

CHADEMA YASIMAMISHA VIONGOZI WAWILI

kashindye

Na Abdallah Amiri, Igunga.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Tabora,kimewasimamisha kazi kwa muda usiojulikana viongozi wake wawili wa Wilaya ya Igunga.

Viongozi waliosimamishwa Mwenyekiti wa Wilaya,Joseph Kashindye na Katibu wake,Idd Athuman.

Akizungumza na waandishi wa habari wilayani hapa jana,Katibu wa Chadema Mkoa wa Tabora, Ally Mwakilima alisema viongozi hao wamesimamishwa uongozi Novemba 30, mwaka huu baada ya kukiuka katiba ya chama hicho.

Alisema uamuzi wa kuwasimamisha ulitolewa na Baraza la Uongozi la Mkoa kwa kile kilichoelezwa kuwa walikiuka na kuvunja Katiba ya chama ibara ya 10:3(4)

Alisema Novemba 28, mwaka huu, viongozi walisimama mbele ya Mahakama ya Wilaya mjini Tabora kutoa ushahidi upande wa mtu aliyeshtaki chama, huku wakiwa wanajua wazi  ni kinyume na ibara ya 10:3 kifungu cha (4) maadili ya wanachama.

Alisema pamoja na kuwasimamisha viongozi hao,baraza hilo limemwagiza Athuman kukabidhi mali zote za chama kwa katibu wa jimbo la Igunga, ikiwa ni pamoja na kujieleza ndani ya siku 14.

Kwa upande wao, Athumani na Kashindye walikiri kupokea barua ya kusimamishwa uongozu Tangu Desemba 3, mwaka huu yenye kumb CDM/M/TBR/WG/01.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles