33.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

RWANDA KUFANYA UCHAGUZI WA RAIS AGOSTI 2017

17008707821_4d25809c36_k

KIGALI, RWANDA

SERIKALI ya Rwanda imetangaza tarehe ya uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri, uchaguzi huo utafanyika Agosti 4, 2017.

Shughuli za kampeni zitaanza Julai, lakini hakuna tarehe rasmi iliyotangazwa kwa wagombea kuwasilisha fomu za kugombea urais pamoja na kuwa taarifa hiyo inasema wagombea watatangazwa kabla ya kuanza kwa kampeni.

Kwa mujibu wa katiba mpya, Rais Paul Kagame anaruhusiwa kuwania muhula wa tatu.

Mtu pekee kutoka kambi ya upinzani aliyetangaza hadi sasa nia yake ya kugombea urais, ni kasisi wa zamani wa Kikatoliki, Joseph Nahimana.

Hata hivyo, juhudi zake za kutaka kurejea Rwanda wiki mbili zilizopita ili kuandikisha chama chake na kugombea urais, ziligonga mwamba.

Kasisi Nahimana na wenzake watatu walikataliwa kuingia Rwanda alipokuwa jijini Nairobi, Kenya akitokea Ufaransa anakoishi kama mkimbizi.

Serikali ya Rwanda haikutaka kuzungumza lolote kuhusu tukio hilo, lakini mashirika ya hapa yanayotetea masilahi ya waathirika wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, walikuwa wameanza kulalamika kuwa tovuti ya Padre Nahimana inaendekeza na kuchochea fikra za mauaji ya kimbari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles