27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

MZEE ANAYESAKA MKE AAPA KUMPATA MWAKA HUU

MZEE Athuman Mchambua (76)
MZEE Athuman Mchambua (76)

Na FARAJA MASINDE-DAR ES SALAAM

MZEE Athuman Mchambua (76) ambaye ametoa tangazo la kutafuta mke wa kuoa, amesema anaamini atafanikiwa lengo lake kabla mwaka huu kumalizika.

Alisema hadi sasa ameshapokea simu za wanawake wa mikoa karibu yote ya Tanzania bara isipokuwa Pwani.

Akizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, Mzee Mchambua alisema kuwa hatatumia tena njia ya kuweka madalali nchi nzima kama alivyoahidi awali, badala yake kuna mkakati mpya ambao anafikiria kuutumia utakaomrahisishia kukamilisha ndoto yake.

“Tangazo tayari limesitishwa tangu Desemba 10, hivyo nimekuwa tu nikiendelea kupokea simu za hapa na pale, japo nazo naona kwa siku mbili hizi kiwango kimeshuka kwani leo (jana) nimepokea simu tatu pekee ikilinganishwa na siku nyingine ambazo nilikuwa nikipokea si chini ya simu sita.

“Kwa sasa nafikiria kutafuta ubunifu mwingine ambao utanirahisishia kumpata mke kabla ya mwaka huu kuisha. Utaratibu huo nitauweka wazi kwenu muda si mrefu ili kila mmoja autambue,” alisema Mzee Mchambua.

Mzee huyo amejipatia umaarufu ndani na nje ya nchi baada ya kuweka tangazo lenye sifa za mke anayemuhitaji mwezi mmoja uliopita kabla ya kuamua kulisitisha baada ya muda wake kumalizika.

Sifa kuu ambazo mzee huyo angependa mke anayemsaka awe nazo, ni pamoja na kuwa na usafi wa hali ya juu, mwenye kushika dini ya Kiislamu, uvumilivu wa ndoa, uwezo wa kilimo, upendo kwa mume, watoto na wajukuu.

Mzee Mchambua ana familia ya mke mmoja ambaye anaishi shamba, watoto 15 na wajukuu kadhaa.

Wiki iliyopita, mzee huyo alitoa masharti mapya kwa mwanamke ambaye atabahatika kuolewa naye. Alisema ataishi naye kwa
miaka mitatu akiwa kwenye kipindi cha uangalizi, na kama atashindwa kutimiza vema masharti hayo, atampa talaka.

Habari za mzee huyo zimezua gumzo katika mitandao na vyombo mbalimbali vya habari vya nje na ndani kutokana na staili ya
aina yake anayoitumia kupata mke amtakaye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles