28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

WAGHANA WAPIGA KURA KUMCHAGUA RAIS WAO

MAHAMA

ACCRA, GHANA

WAPIGAKURA nchini hapa, leo wanatarajia kumchagua rais atakayewaongoza kipindi cha miaka minne, huku mgombea mkuu wa upinzani, Nana Akufo-Addo, akisema demokrasia ya Ghana iko njia panda.

Hii ni mara ya pili kwa Rais John Mahama wa Chama tawala cha National Democratic Congress (NDC) kumkabili Akufo-Addo, kiongozi wa chama cha New Patriotic Party (NPP), ambaye anafanya jaribio lake la tatu na linaloelekea kuwa la mwisho kuwania nafasi hiyo.

Mwaka 2012, Mahama alipata ushindi mwembamba wa asilimia 50.7 dhidi ya asilimia 47.7 ya kura alizopata Akufo-Addo (72), ambaye bila mafanikio alipinga ushindi huo mahakamani.

Mahama (58) ana faida ya kuwa rais mtetezi na ametumia fedha nyingi katika miradi ya miundombinu kuelekea siku ya uchaguzi.

Aliingia madarakani mwaka 2012 baada ya kifo cha ghafla cha mtangulizi wake, John Atta Mills na amebakia maarufu akihesabiwa kama mtu wa watu.

Lakini amelazimika kutetea uongozi wake kutokana na mdororo wa uchumi na mlolongo wa kashfa za ufisadi, ikiwamo iliyosababisha kutimuliwa kwa majaji zaidi ya 20 mwaka 2015.

Akufo-Addo amekishutumu chama tawala kujaribu kuchochea ghasia, huku polisi wakifumbia macho suala hilo na kutia doa taifa hilo ambalo kwa muda mrefu limetambulika kama ‘kitovu cha demokrasia Afrika’.

“Kwa sasa tuko vibaya… Itakuwa bora visa vya ghasia vinavyosababishwa na mitandao ndani ya chama tawala vikabiliwe kwa mujibu wa sheria,” Akufo-Addo aliwaambia wanahabari nyumbani kwake baada ya kampeni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles