29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mabilioni yaliyofichwa Uswisi yachunguzwa

masajuElias Msuya na mashirika ya habari ya kimataifa
WAENDESHA mashtaka nchini Uswisi wamevamia katika ofisi za benki ya HSBC iliyopo Geneva na kuanza kuhoji madai ya fedha zilizopo kinyume na sheria katika benki hiyo.
Hivi karibuni mtandao wa Swiss Leaks chini ya Waandishi wa Habari za Uchunguzi wa Kimataifa (ICIJ) ulifichua kuwepo kwa Watanzania 99 wenye akaunti za siri nchini humo zenye zaidi ya Sh 205 bilioni na kwamba Tanzania ni nchi ya 100 kwa nchi zenye fedha nyingi nchini Uswisi.
Hata hivyo akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju (AG) alisema kamati iliyoundwa na ofisi yake kuchunguza mabilioni ya fedha yaliyofichwa na baadhi ya Watanzania katika benki mbalimbali nchini Uswisi imekamilisha uchunguzi na inasubiri kukabidhi ripoti ya kazi hiyo kwa Spika wa Bunge.
Taarifa kutoka mashirika ya habari ya kimataifa zinasema kuwa waendesha mashitaka hao wa polisi walikuwa wakipeleleza benki hiyo na watu wasiojulikana wanaotuhumiwa kuhusika na utoroshaji wa fedha.
“HSBC ilisema itashirikiana na mamlaka za Serikali ya Uswisi,” ilisema taarifa ya BBC.
Baada ya mtandao wa Swiss Leaks kutoa taarifa yake, benki ya HSBC ilichapisha matangazo kwenye kurasa za magazeti ikiomba radhi kwa madai hayo.
Ofisa Mtendaji mkuu wa benki hiyo, Franco Morra alisema wiki iliyopita kwamba wameamua kufunga akaunti za wateja wasiofikia vigezo vyao.
Morra aliongeza kuwa kuibuka kwa suala hilo la kihistoria katika biashara imekuwa ni tahadhari kwamba mfumo wa kizamani wa biashara unaofanywa na benki binafsi za Uswisi haukubaliki tena.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Naibu Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba alisema serikali inalifuatilia suala hilo kupitia Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) na Financial Intelligence Unit (FIU).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles