25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Lukuvi amwakilisha JPM mazishi ya Mungai

Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho katika jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu na Ufundi, Joseph Mungai, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika Mafi nga mkoani Iringa jana.
Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho katika jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu na Ufundi, Joseph Mungai, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika Mafi nga mkoani Iringa jana.

NA RAYMOND MINJA, IRINGA

VIONGOZI mbalimbali, wakiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, jana walishiriki kumzika waziri wa zamani na mwanasiasa mkongwe nchini, Joseph Mungai, nyumbani kwake wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.

Mungai, aliyezaliwa Oktoba 24, 1943, alifariki dunia  Novemba 8, mwaka huu, jijini Dar es Salaam  baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Akizungumza katika ibada ya mazishi, Waziri wa Ardhi, Nyumba Maendeleo ya Makazi, Wiliamu Lukuvi, aliyemwakilisha Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, alisema  Mungai atakumbukwa kwa uongozi wake uliotukuka, hasa katika misingi mizuri ya Elimu ya Sekondari (MMES.

Lukuvi alisema wakati Serikali ilipoanzisha suala la Sekondari za Kata, Mafinga na Mufindi kwa ujumla mwamko huo ulishaanza toka miaka ya 1980, ambayo kwa uongozi wake kama Mbunge alihamasisha wananchi kutoa michango, kufyatua matofali na kina mama kuchota maji, yote hiyo ni katika kufanikisha azma ya kusogeza elimu ya sekondari kwa watu wengi.

“Alianza kuwa kiongozi akiwa na umri mdogo kuliko wanasiasa wote wa Mkoa wa Iringa wakati huo, lakini pia alikuwa kiunganishi pale kunapotokea misuguano yoyote, hakuwa na makuu na kama ulikuwa ukitaka ushauri basi utaupata kwa mzee wetu Mungai,” alisema.

Akiongoza ibada ya mazishi,  Askofu  wa KKKT Dayosisi ya Iringa, Odenbang Mdegeka, alisema kila mwanadamu aishie chini ya hili jua anapaswa kuishi maisha ya kumuabudu Mungu na kuachana na tabia ya kuhukumiana hapa duniani, kwakuwa kila mtu atajibu dhambi zake akiwa mbinguni.

Mdegela alisema Mungai ni kati ya viongozi wachache walioacha historia kubwa hapa nchini, kutokana na uongozi wake uliotukuka wa kupigania maendeleo ya Watanzania bila ubaguzi wa aina yoyote.

“Leo tumempoteza mtu muhimu sana ndugu yangu Lukuvi, mimi na wewe tunapaswa kukaa chini na kuangalia mustakabali wa mkoa wetu wa Iringa, ameondoka mzee Siyovvela,  ameondoka Adam Sapi na leo ameondoka mzee wetu Mungai, sasa ni wakati wetu, kwani kwa Iringa tumebaki mimi na wewe, sasa tukutane kabla mwaka haujaisha ili kujadili jambo hili,” alisema Mdegella.

SUMAYE

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, alisema Taifa limempoteza kiongozi makini aliyekuwa na uthubutu wa kutenda mambo bila ubaguzi na kusimamia kile anachokiamini katika kuwatumikia Watanzania.

Alisema Mungai alikuwa ni mtu mchapakazi aliyekuwa na hoja alizozijenga na kuzisimamia kikamilifu, kwani alitamani sana kutenda mambo kwa haki bila kubaguana kiitikadi, bali alisimama katika haki.

Alisema Chadema kimesikitiswa sana na kifo chake, kwani alikuwa ni mtu mpenda demokrasia, hivyo katika kumuenzi na kutambua mchango wake hapa nchini, wataendeleza kudumisha misingi mizuri ya demokrasia aliyokuwa akiishi marehemu Mungai.

Luhavi

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Rajabu Luhavi,  alisema Mungai atakumbukwa kwa uongozi wake uliotukuka kwakuwatumikia Watanzania bila ubaguzi.

“Alikuwa kiongozi mzuri tangu uongozi wa hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Ametoa mchango mkubwa kwenye maendeleo ya nchi yetu, tunapaswa kuenzi yale mazuri waliyoyafanya na sisi tunaanzia pale  alipoishia.”

Akizungumzia wasifu wa marehemu, Denis Mungai alisema kuwa Mungai  aliwahi kuwa Mbunge wa Mufindi kupitia CCM kwa miaka 35.

Pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini enzi za utawala wa hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na pia katika awamu za pili, tatu na nne.

Baadhi ya nyadhifa alizowahi kushika kwa nyakati tofauti ni uwaziri wa iliyokuwa Wizara ya Elimu na Utamaduni, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. katika utawala wake, Mungai alifuta Umoja wa Michezo wa Shule za Msingi (UMISHUMTA) na Umoja wa Wabunge.

Baadhi ya wabunge wa majimbo ya Mkoa wa Iringa walizungumzia Mungai, huku kila mmoja akisema alikuwa kiongozi mkweli aliyesimamia alilokuwa analiamini.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi, alisema watu wa Mafinga na Mufindi kwa ujumla wamempoteza mtu muhimu sana, kwani atakumbukwa kwa mengi aliyofanya, hasa mwamko na kuisogeza elimu ya sekondari kwa watu wa kawaida kupitia Mufindi Education Trust-MET.

Chumi alisema wakati Serikali ilipoanzisha suala la Sekondari za Kata, Mafinga na Mufindi kwa ujumla mwamko huo ulishaanza toka miaka ya 1980, ambayo kwa uongozi wake kama Mbunge alihamasisha wananchi kutoa michango, kufyatua matofali na kina mama kuchota maji katika kufanikisha azma  ya kusogeza elimu ya sekondari kwa watu wengi.

“Kwa jitihada za mzee Mungai Mufindi ndiyo Wilaya ya Kwanza hapa nchini kuwa na Benki ya Wananchi, yaani Community Bank (Mucoba), ambayo imeendelea kuwa kimbilio la tabaka la chini na kati katika suala zima la mikopo na huduma za kibenki. Mimi nawaombea faraja wanafamilia wote katika kipindi hiki cha majonzi, Mungu ailaze Roho yake Mahali Pema Peponi, Amina,” alisema Chumi.

MSIGWA

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), alisema Mungai alikuwa kiongozi wa wazi asiyegopa kusimamia ukweli.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles