Wafanyabiashara mbali mbali nchini wametakiwa kuacha kuweka fedha majumbani badala yake waweke fedha hizo katika kadi za kibenki ili kuwa na usalama wa fedha zao.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Data Vision, Maclen Gmwaijonga, amesema kuweka fedha katika kadi ni njia bora zaidi na salama kuliko kuweka fedha ndani.
“Kumekuwa na wizi mkubwa wa fedha na hii yote inatokana na usalama wa uwekaji wa fedha,” alisema Gmwaijonga.
Alisema tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo mwaka 1998 mpaka sasa zaidi ya benki 35 na taasisi za kifedha zimejiunga na Data Vision kibishara kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
Alisema licha Tanzania kukua kiteknolojia bado ipo chini katika kwa matumizi ya kadi za kibenki katika suala zima la ufanyaji wa biashara hii inatokana na kukosa kwa uelewa wa huduma hizo, hivyo eimu zaidi inahitajika.