26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi 16 waachishwa shule kwa ujauzito

ujauzitoNa Safina Sarwatt-Moshi

WANAFUNZI 16 wa shule za msingi na sekondari katika Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, wameachishwa masomo mwaka huu baada ya kubainika kuwa na ujauzito na kulazimishwa na wazazi wao kuolewa.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu jana wakati wa kikao na maofisa elimu wa wilaya hiyo.

Alisema tatizo la wanafunzi kuachishwa masomo baada ya kupata ujauzito ni kubwa, hali hiyo inasababisha wanafunzi kushindwa kufikia ndoto ya kupata elimu.

“Kutokana na kushamiri kwa vitendo hivyo, Serikali ya wilaya imeweka utaratibu wa kuwakamata wazazi wote ambao watabainika kuachisha masomo watoto wao kwa ajili ya kuwaozesha kwa vigezo vya kuendeleza mila,” alisema.

Kwa upande wake, Ofisa Elimu Kata ya Karansi, Rosemary Mhindi, alisema tatizo kubwa linalokwamisha wanafunzi kutoendelea na masomo linatokana na wazazi wao, hususani wale wa jamii ya wafugaji kuwataka watoto wao kufanya vibaya ili kuwaozesha.

“Elimu bado inahitajika kwa jamii ya wafugaji kuhusu umuhimu wa elimu kwa watoto wa kike,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles