32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wachina kortini kwa kumteka mwenzao

hukumuNa KULWA MZEE – DAR ES SALAAM

RAIA watatu wa China wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka mawili likiwamo la kumteka mwenzao.

Washtakiwa hao ambao walifikishwa mahakamani hapo jana na kupandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha ni  Chen Bao (34), dereva Wang Jian (37) na mfanyabiashara Zheng Pa Jian au Mr. Ping.

Upande wa jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Hellen Moshi, uliwasomea washitakiwa hao mashitaka ya kumteka mwenzao na kumjeruhi kwa kumpiga katika matukio yaliyotokea maeneo ya Palm Beach, wilayani Ilala, Dar es Salaam.

Mshitakiwa Bao alikiri kumteka mwenzake na kumjeruhi huku Jian akikiri kosa la kumjeruhi  na Mr. Ping alikana kutenda makosa hayo.

Akiwasomea mashtaka hayo, Hellen alidai washtakiwa walitenda makosa hayo,  Oktoba 21, mwaka huu, katika maeneo ya Palm Beach, wilayani Ilala, Dar es Salaam.

Alidai katika shtaka la kwanza, washitakiwa hao siku hiyo walimteka Liu Hong kwa nia ya kumweka kwenye hali ya hatari kwa mauaji.

Shtaka la pili, ilidaiwa siku hiyo katika eneo hilo, washtakiwa hao  walimpiga Liu sehemu mbalimbali za mwili wake, hivyo kumsababishia majeraha mwilini.

Baada ya washtakiwa kusomewa mashtaka hayo, ambayo  Bao alikiri kumteka mchina mwenzake na kumjeruhi huku Jian akikiri kosa la kumjeruhi  na Mr. Ping alikana kutenda makosa hayo, Wakili alidai upelelezi haujakamilika.

Hellen  aliomba shauri hilo kuahirishwa na kwamba wamewasilisha mahakamani hapo hati ya kupinga dhamana dhidi ya washtakiwa hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles