26.5 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

BMT yapiga ‘stop’ ukodishwaji Yanga, hisa Simba

 Mohamed Kiganja
Mohamed Kiganja

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

BARAZA la Michezo Taifa (BMT), limesitisha michakato yote inayoendelea ndani ya klabu ya Simba na Yanga, kubadili umiliki wa timu kutoka kwa wanachama kuelekea kwenye umiliki wa hisa na ukodishwaji, hadi hapo watakapofanya marekebisho ya katiba zao.

Uamuzi huo wa Serikali unakuja huku klabu ya Yanga ikiwa tayari imeingia mkataba wa miaka 10 wa ukodishwaji na Kampuni ya Yanga Yetu Limited, Septemba mwaka huu, wakati Simba ikiwa katika hatua ya mwisho kumkabidhi klabu hiyo mfanyabiashara, Mohammed Dewji ‘Mo’ kwa umiliki wa hisa za asilimia 51.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Mohamed Kiganja, alisema michakato hiyo itaendelea kwa wahusika kufuata sheria na taratibu za nchi katika kufikia lengo lao.

“Hivi karibuni imeibuka michakato ya watu wakitaka kubadili umiliki wa klabu za wananchi na kuzielekeza kwenye utaratibu wa hisa na ukodishwaji.

“Vitendo hivyo vimesababisha migogoro ambayo inaashiria uvunjifu wa amani ndani ya tasnia ya michezo,” alisema Kiganja.

Kiganja aliongeza kuwa kwa sasa makundi ya wapenzi na wanachama wa soka yamejikita zaidi katika mijadala ambayo hatima yake ni kuzidi kuibomoa jamii badala ya kuijenga na kuimarisha michezo nchini.

“Mpasuko huo umesababisha baadhi ya wanachama ambao hawaridhishwi na mwenendo mzima, kukiuka taratibu za suluhu zilizopo ndani ya klabu zao na kuamua kukimbilia mahakamani.

“Athari za migogoro hiyo kupelekwa mahakamani ni kubwa kwa klabu zetu na Shirikisho la Soka (TFF), hivyo kutokana na hali hii, BMT haiwezi kuvumilia ukiukwaji wa sheria na taratibu unaoendelea ambao unaashiria kutoweka kwa amani kwenye tasnia ya michezo,” alisema Kiganja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles