25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wagombea umakamu rais wachuana katika mdahalo Marekani

57f4774e3b74d-image

NEW YORK, MAREKANI

WAGOMBEA wawili wa umakamu wa rais nchini Marekani wameshambuliana kwa maneno makali katika mdahalo wa televisheni, kila mmoja akimshambulia mwenzake juu ya mgombea wake wa urais na sera zao.

Ikiwa ni wiki tano kabla ya Uchaguzi Mkuu wagombea hao wenza kutoka chama cha Democrat, Tim Kaine na Republican, Mike Pence walirushiana vijembe vilivyoegemea zaidi kuhusu wagombea urais wao, Hillary Clinton na Donald Trump.

Wakati kila mmoja alikuwa akijisifia kuhusu uwezo alionao binafsi, kila upande uliwakingia kifua wagombea wao wa urais kuelekea uchaguzi wa Novemba 8.

Kura za maoni zinaonesha Clinton amejiongezea umaarufu katika kipindi cha wiki iliyoonekana kumpa funzo mpinzani wake wa Republican, Donald Trump ambaye amekuwa akiandamwa na utata kuhusu kukwepa kodi pamoja na jinsi anavyowatendea wanawake.

Kaine, ambaye ni Seneta wa Virginia, akiwa mgombea umakamu wa rais wa Chama cha Democrat alimuandama Trump tangu mwanzoni mwa mdahalo akisema fikra ya kumuunga mkono mgombea huyo kuwa amiri jeshi mkuu inatia hofu kubwa.

Siwezi kuamini ni vipi Gavana Pence anavyoweza kumtetea mtu kama Trump ambaye amejawa na kiburi, matusi na nadharia ya kujipendelea, aliongeza Kaine.

Kadhalika mgombea huyo wa Democrat amejitapa kuwa yeye ni mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa ya ndani ya jimbo lake, na taifa kwa ujumla.

Aliendelea kusema kuwa yu mtu sahihi kuwa makamu rais wa Clinton aliyemtaja kuwa mwanamke anaweza kuaminika na mwenye uwezo mkubwa wa kuwa amiri jeshi mkuu wa Marekani.

Hata hivyo kwa upande wa mgombea wa chama cha Republican ambaye ni Gavana wa Indiana,  Mike Pence aligeukia suala zima la sera za nje za Clinton akimshambulia hasa juu ya Mashariki ya Kati.

Alisema “Tunaiona takriban nusu ya dunia nzima na hasa eneo kubwa la Mashariki ya Kati ikishindwa kudhibitiwa.

Hali tunayoishuhudia  saa baada ya saa nchini Syria leo hii ni kutokana na  sera dhaifu za nje ambazo Hillary Clinton alisaidia kuundwa kwake na utawala uliopo sasa madarakani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles