26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

TBL Group yageukia elimu unywaji kistaarabu

roberto-jarrinNa HERIETY FAUSTINE

-DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya TBL Group imeanza kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya jamii juu ya umuhimu wa unywaji wa pombe kistaarabu ili kuepusha madhara yatokanayo na matumizi ya vinywaji vyenye kilevi kupita kiasi.

Ujumbe huo wa kampuni ulitolewa katika kipindi cha Wiki ya Nenda kwa Usalama, ikiwa ni mmoja wa wadau wa kuendesha kampeni za usalama barabarani na katika sehemu za kazi na kwenye jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group, Roberto Jarrin, alisema elimu ya unywaji wa kistaarabu pia ni moja ya maazimio yaliyofikiwa na makampuni ya kutengeneza bia na vinywaji vingine yenye kilevi katika nchi 76 duniani katika maadhimisho ya ‘Siku ya Unywaji Kistaarabu Duniani’. Kampuni hizo zimeazimia kushirikiana na Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na wafanyakazi wake na wateja wanaotumia vinywaji hivyo kufanikisha kampeni ya unywaji wa kistaarabu.

“Tukiwa ni watengenezaji wa bia na vinywaji vingine vyenye kilevi, ni wajibu wetu pia kuwaelimisha wateja wetu kuvitumia kistaarabu kwa afya na si kwa kuleta madhara ikiwemo kushindwa kushiriki katika shughuli za uzalishaji kwa sababu ya ulevi,” alisema Jarrin.

Mkurugenzi wa mafunzo wa TBL Group, Gasper Tesha, alisema kampuni imekuwa ikitoa mafunzo kwa wafanyakazi wake na  makundi mbalimbali ya jamii na inaendelea kuwafikia wananchi wengi kwa njia  ya semina, vyombo vya habari na vipeperushi na sehemu zenye mikusanyiko ya watu pamoja na sehemu za kuuzia vinywaji.

Alisema moja ya malengo ya kampuni ni kuhamasisha unywaji wa kistaarabu na kuhakikisha jamii haipati athari kutokana na matumizi ya vinywaji vyenye kilevi, bali watumiaji wanapaswa kunywa kiasi kwa ajili ya kujiburudisha na kujenga afya zao.

“Elimu hii tayari imeingizwa katika mafunzo ambayo kampuni inayatoa kwa wajasiriamali wanaouza bidhaa zetu ijulikanayo kama Retail Development Progamme yanayoendelea nchi nzima, tuna imani kupitia njia hii itawafikia watumiaji wengi wa bidhaa zetu,” alisema Tesha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles