28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Hatima kesi ya Murunya na wenzake kujulikana leo

murunyaNa JANETH MUSHI – ARUSHA

HATIMA ya aliyekuwa Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Benard Murunya na wenzake watatu kama wana kesi ya kujibu au  hawana, inatarajiwa kutolewa leo na Mahakama ya Wilaya ya Arusha.

Murunya ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), ameshtakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia NCAA upotevu wa dola za Marekani 66,890 sawa na Sh milioni 133.7.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo, ni aliyekuwa Meneja wa Utalii NCAA, Veronica Funguo, aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mamlaka hiyo, Shad Kiambile na Mkurugenzi wa Kampuni ya Cosmos ya Uwakala wa Usafirishaji, Salha Issa.

Uamuzi wa kesi hiyo ulikwama kutolewa mara mbili. Julai 19, mwaka huu, ulishindikana kutolewa baada ya hakimu Patricia Kisinda wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha kudaiwa kuumwa na Agosti 10, mwaka huu kukwama tena baada ya hakimu huyo kudaiwa kuwa likizo.

Katika kesi hiyo, upande wa Jamhuri uliwakilishwa na mawakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Arusha, Wakili Mwandamizi, Rehema Mteta na Hamidu Sembano, wakati Murunya na wenzake, wakitetewa na wakili John Materu na Boniface Joseph.

Murunya na wenzake, wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao na kuisababishia mamlaka hiyo upotevu wa dola 66,890, ikiwa ni pamoja na kuipatia Kampuni ya Cosmos fedha hizo kabla ya kutoa huduma, kinyume cha sheria ya matumizi ya fedha za umma, huku fedha hizo zikidaiwa kutotumika kwa kazi iliyokusudiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles