Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe imepata gari la zimamoto kukabiliana na majanga ya moto katika wilaya hiyo inayozungukwa na visiwa zaidi ya 30 ndani ya Ziwa Victoria.
Kamishna Msaidizi wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza, James Mbate, alieleza kwamba gari hilo limetolewa na Serikali ya  Japan kwa lengo la kukabiliana na majanga ya moto yatakapojitokeza ukizingatia jiografia ya wilaya hiyo kuwa na visiwa vingi.
Kamanda alisema Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Estomih Chang’a na Mkurugenzi wa Halmashauri ya hiyo, Tumain Shija wameahidi kutoa fedha za kulikamilishia mfumo wa tanki la maji wa gari hilo haraka iwezekanavyo.