25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Dany Kidega awa Spika EALA

Margaret-ZziwaNa Elizabeth Mjatta
MBUNGE wa Chama cha National Resistance Movement (NRM) cha Uganda, Dany Kidega amechaguliwa kuwa Spika mpya wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
Kidega anachukua nafasi ya aliyekuwa Spika wa Bunge hilo, Dk. Margareth Zziwa, aliyeondolewa kutokana na kukabiliwa na kashfa mbalimbali.
Kidega alipata ushindi huo baada ya mbunge mwenzake kutoka Uganda Christopher Okumu (UPC), kujiengua katika kinyang’anyiro hicho muda mchache baada ya kuingia bungeni.
Baada ya Dk. Zziwa kung’olewa katika wadhifa huo, Okumu, alikaimu nafasi hiyo hadi kuibuka kidedea katika uchaguzi wa jana.
EALA juzi lilimuondoa madarakani Dk. Zziwa kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kushindwa kutimiza wajibu na matumizi mabaya ya madaraka.
Kuondolewa kwa Dk. Zziwa kulitokana na wabunge wa EALA kupiga kura na 36 kati ya 39 waliohudhuria kikao cha dharura kilichofanyika juzi chini ya uenyekiti wa Kaimu Spika, Okumu, walipiga kura za ndiyo kukubali hoja ya kumuondoa madarakani.
Wabunge wawili walipiga kura ya hapana, wakati mmoja hakupiga kura hoja hiyo iliyowasilishwa Machi, mwaka huu na Mbunge wa Kenya, Peter Mathuki na kuibua mvutano miongoni mwa wabunge waliokuwa wakimtetea Dk. Zziwa na wale waliotaka ang’oke.
Uamuzi wa kumng’oa Dk. Zziwa umechukuliwa kwa kuzingatia kifungu cha 53(3) cha Katiba ya kuanzishwa kwa EAC, inayowapa mamlaka wabunge kumwondoa ofisini spika.
Baada ya kung’olewa katika nafasi hiyo baadhi ya wabunge walifurahia na kusema wamefanikisha walichokihitaji kwa muda mrefu.
Dk. Zziwa alisimamishwa wadhifa wake kutokana na hoja iliyopitishwa na wabunge wa EALA Novemba, mwaka huu katika kikao chake cha Mjini Nairobi akizuiwa kutekeleza majukumu yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles